DANIELI 2:1-49
UNTANGULIZI
Danieli alimpa Mungu utukufu alipomweleza mfalme tafsiri ya ndoto yake. Danieli alipompa Mungu utukufu, naye mfalme Nebukadneza alimpa Mungu wa Danieli utukufu. Tutakuwa na jumbe kadhaa katika Daniei mlango wa pili. Leo hii twatazama kanuni alizotumia Danieli wakati wa changamoto za maisha yake. Jumapili iliyopita tuliona Danieli mtu wa kuazimu. Pia tuliona maana ya majina ya vijana wane. Danieli– Mungu ndiye hakimu wangu (God is my judge) Hanania– Mungu ni mwenye neema (God is gracious) Misheali– Mungu hafananishwi (God is without equal) Azaniah– Mungu ni msaidizi wangu (God is my helper). Leo tunatazama ndoto ya mfalme Nebukadneza na kijana Danieli ambaye kwa nguvu za Mungu aliyaokoa maisha yake na ya wezake na kumpa Mungu utukufu.
Hebu tujifunze:-
I. CHANGAMOTO YA DANIELI NA WENZAKE (Danieli 2:1-13)
- Danieli alijikuta katika chnagamoto tena.
- Danieli sasa alikuwa moja wa Wakaldayo, wenye hekima katika jumba la mfalme.
- Danieli alikuwa anaendelea kufanya kazi akiwa mwaminifu kwa Mungu na kwa mfalme.
- Kuokoka na kuwa mwaminifu kwa Mungu si kusema shida na changamoto hazitakuwa.
- Yesu Kristo aliteswa, wanafunzi wake wengine waliuliwa mauti ya huzuni sana.
- Manabii wa zamani waliuliwa, Danieli alitupwa katika tundu la simba.
- Mfalme Nebukadneza aliota ndoto ndiposa ameisahau ndoto lenyewe na tafsiri hana !
- Danielei alimwambia mfalme kwamba hakuna mtu angaliweza kujua ndoto ya mfalme na kutafsiri!
- Hivyo wote wenye hekima na pomoja na Danieli watauliwa (V.12-13)
II. MPANGO WA DANIELI (2:14-16)
- Danieli alipambana na hali kwa njia ya kiungu.
- Danieli hakufadhaika hau kukasirika, lakini alifuata kanuni za Mungu.
- Danieli kwanza alitafuta habari kamili juu ya jambo hilo (He gathered information)
- Danieli aliomba apewe wakati zaidi.
- Huu ni wakati wa kuomba Mungu wake.
- Danieli hakufadhaika na kuwalaumu watu, lakini alimwamini Mungu na Kumtengemea yeye.
III. MAOMBI YA DANIELI (2:17-23)
- Danieli aliomba– Danieli alienda nyumbani, Danieli aliwaeleza wenzake (Hanania-Mungu ni mwenye neema), Mishaeli (Mungu hafananishwi) Azaria (Mungu msaidizi wangu)
- Danieli aliwaomba wote wautafute uso wa Mungu.
- Maombi yao ilivunja fadhaa zao– Mungu anajibu maombi.
- Mungu aliwapa Amani katikati ya dhiki kuu– Amani.
- Maisha ni vita-maombi ni kilio kwa Mungu anayeweza yote (Wafilipi 4:4-6)
- Danieli alimsifu Mungu kwa kuyajibu maombi (v.20-23)
IV. TANGAZO LA DANIELI (2:27-28; 45)
- Mungu mkuu alimwonyesha mfalme Nebukadneza yatakayo tendeka duniani.
- Ndoto yako ni hakika na tafsiri yake ni dhabiti (45)
- Danieli alimpa Mungu utukufu wote.
- Naye mfalme Nebukadreza alimpa Mungu wa mbinguni utukufu na sifa (v.46)
V. DANIELI AKATUKUZWA AKAPANDISHWA CHEO (2:46-49)
- Danielei alipanda cheo (Mathayo 25:23) uaminifu ni bora
- Uaminifu kazini, nyumbani, shuleni ndio chanzo cha kupandishwa cheo.
- Hivyo Mungu alitukuzwa na Danieli alipandishwa cheo, wenzake Danieli na wao walipata mamlaka huko Babeli.
MWISHO
- Mtu hasipo ungana na mbingu hawezi kuona maono, ndoto, unabii– anaona bure, anasikia bure. Kila kitu katika ulimwengu wa Roho inakuwa giza tupu, kiziwi na bubu– wakati huo mtu anaitaji ukombozi.
- Utafsiri wa maono na ndoto unahitaji Roho mtakatifu.
- Changamoto zako zinaitaji maombi ya Imani na usaidizi kutoka mbinguni.
- Leo kuna msaada kutoka juu mbinguni kwa ajili yako.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
