DANIELI 2:31-45
UTANGULIZI
Daniel- (Mungu ni hakimu wangu) Hananniah (Mungu ni mwenye neema) Mishaeli (Mungu halinganishwi) Azariah (Mungu ndiye anisaidiaye).
Danieli akawa mtu wa maono, ndoto, unabii na mtafsiri wa akili na mausia ya Mungu. Maono ya mfalme Nebukadreza yalitisha sana. Furaha ya wasio na Mungu inharibika haraka, kwa ndoto yake mfalme alifadhaika sana. Ndoto yake ilitoweka kutoka kwa akili zake, hivyo akataka kufahamishwa na mwenye hekima (v.5). Jambo hili lilikuwa ngumu Zaidi lakini, lisilo wezekana kwa mwanadamu, linawezekana kwa Mungu (v.10). Mungu wa Danieli anayafahamu yote na uwezo wake hauna kifani.
Nebukadreza aliona na tazama sanamu kubwa sana, sanamu hii pia ilikuwa na mwangaza mwingi sana, sanamu hii pia ilitisha sana. Mungu alionyesha Enzi za utawala wa mwanadamu (gentile rule)
- Kichwa cha dhahabu safi– ufalme wa babeli-Nebukadreza– Enzi yake ilikuwa ya uwezo,nguvu na utukufu.
- Ufalme na enzi ya Nebukadreza (606 BC-539.BC)
- Kifua na mikono ya fedha– Medo– Persia (Mende na Uajenzi) 539BC-331BC. Dario na Koreshi.
- Tumbo na viuno vya shaba-wagiriki (Greece)-331BC-146BC. Alexander the Great na jemedari wake wanne.
- Miguu ya chuma– Roma– 146 BC– AD 476– Ufalme wa Kaizari– Roman Catholic church.
- Nyayo za miguu– Nusu chuma na nusu udongo. European Union-Inchi maskini na inchi tajiri katika muugano AD.476-mpaka leo (25Nations)
- Jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, jiwe likaipiga sanamu miguu yake, likaivunja vipande vipande.
- Upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake.
- Leo tunatazama hili Jiwe la zamani– Yaani Kristo– Jiwe mfano wake ni Kristo. Kristo ataipiga sanamu ya enzi zote za mwandamu. Mahali pake pasionekane tena (v.34,35,44)
- Yesu Kristo ni mwamba na jiwe, hivyo yeye ni mwenye nguvu na kudumu milele.
I. KAMA JIWE ISRAELI WANAKWAZIKA JUU YA KRISTO (Mathayo 21:42-44)
- Yesu Kristo kwa Israeli ni “Jiwe la kukwazika” (Zaburi 118:22-24, Matendo 4:10-12, Warumi 9:33, I Petro 2:6-8)
- Yesu Kristo alikuwa kama mtumishi na kama jiwe alidharauliwa sana na waashi wa Israeli.
- Hata ingawa Mungu alimtoa Yesu Kristo kuwa msingi wa Ziyuni (Isaya 28:16)
- Israeli walianguka juu la Jiwe hilo– Taifa lao likavunjika vunjika (Mathayo 21:44)
- Israeli wakatawanyika duniani kote mpaka leo.
II. KAMA JIWE KANISA LIMEJENGWA JUU YA KRISTO (Mathayo 16:16-18)
- Kanisa la kweli limesimama juu ya Jiwe– Yesu Kristo.
- Nguvu za kuzimu haziwezi kamwe kuivunja kanisa.
- Yesu Kristo ni jiwe la pembeni (Matendo 4:10-11)
- Familia, ndoa na maisha tujenge juu ya jiwe hili.
- Tumjie Kristo kama jinsi “Jiwe lililo hai (Living Stone) I Petro 2:4.
- Kristo ni yeye mwanzilishi wa uzima wa milele.
- Hakuna msingi na jina linguine– Yesu Kristo pekee!!
III. KAMA JIWE NGUVU ZA MATAIFA ZITAVUNJWA NA KRISTO (V.34)
- Jiwe hili lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono.
- Mataifa yote yatakwisha kwa haraka nyingi sana.
- Mataifa yote ya dunia hii yatakwisha bila mapambano ya mwanadamu (Mathayo 21:44)
- Hakutakuwa na uchanguzi tena, hakuna maraisi, mawaziri, mbunge, seneti, magavana etc.
- Ufalme huu wa kristo utakuwa wa milele na milele, hakuna kurithiana (No Succession)
- Ufalme wa Mungu utakuja kama umeme na kama mwivi usiku (Mathayo 24:12)
- Kristo hatakuja tena kama mtoto katika hori ya ngombe.
- Kristo atarudi kama mfalme, mataifa yote yavunjika vunjika.
IV. KAMA JIWE ULIMWENGU UTAJAA UTUKUFU WA KRISTO.
- Kurudi kwa Yesu Kristo hakutakuwa mwisho wa ulimwengu lakini mwanzo wa enzi ya Kristo.
- Jiwe hilo litajaza dunia yote (v.35)
- Ufalme wa Yesu Kristo utakuwa bila ufisadi
- Utukufu wake utajaa kila mahali (Zaburi 72)
- Falme na Mataifa yote yatakuwa chini ya Kristo, Jina lake litakuwa juu ya majina yote, mataifa yote yatamwita barikiwa. Hallelujah!
MWISHO
- Je, umejenga maisha yako juu ya Jiwe hilo?
- Je, ukotayari kutawala pamoja na Kristo?
- Maranatha!! Joo upesi Bwana wetu– Ameni
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
