2 MAMBO YA NYAKATI 19-20
UTANGULIZI
Hata ingawa mfalme Yehoshafati alijifunga kongwa moja na wasio amini, na akapona mauti katika vita, tunaona kwamba Yehoshafati alimrudia Mungu wake. Yehoshafati alirudi Yerusalemu kwa aibu nyingi. Mara tu alipoingia nyumbani kwake Yerusalemu, Yehu mwana wa Hanani, Mwonaji alikwenda kumlaki akamwambia “Je! Imekupasa kuwasaidia waovu na kuwapenda wamchukiao Bwana ?”. (19:2). Lakini jambo moja lilikuwa nzuri kwa moyo wake mfalme Yehoshafati “Moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu” (19:3). Tumeona njia yake kuteremkia dhambi na aibu. Dhambi huleta Aibu. Leo tunaona njia ya kumrudia Mungu na kutubu:-
I. YEHOSHAFATI ALIWARUDISHA WATU KWA BWANA (19:4)
- Watu wa Yuda tayari walikuwa wamerudi nyuma kwa sababu ya mfano mbaya wa mfalme Yehoshafati.
- Kuna watu wanasimama kwa sababu wewe umesimama.
- Ukianguka na wao wanaanguka, ukifanyadhambi na wao wanafanya dhambi.
- Wewe in nuru ya ulimwengu (Mathayo 5:13-16)
- Wamebarikiwa wanao warundisha watu kwa Mungu (Daniel 12:3)
- Twahitaji kuwarudisha watu kwa Mungu si tu kuwarundisha kwa kanisa.
II. YEHOSHAFATI ALIWAFUNDISHA NJIA ZA MUNGU (19:7)
- Hofu ya Bwana na iwe juu yenu
- Mungu hana ouvu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
- Mungu wetu hapokei rushwa, simheshimu watu, hapokei zawadi.
- Yehoshafati alijifundisha mengi kutoka kwa mfalme Ahabu (Kumbu kumbu 32:4)
III. YEHOSHAFATI ALIWAONYA JUU YA DHAMBI YA KURUDI NYUMA (19:10)
- Yehoshafati alijifunza kwa ujuzi, kwamba dhambi huleta karibu ghadhabu ya Mungu
- Kwenda mbali na Mungu ni dhambi na dhambi huleta majuto.
- Mbali na mapenzi ya Mungu ni uwanja ulio katazwa.
IV. YEHOSHAFATI ALITAFUTA MSAADA WA MUNGU SIKU YA TAABU (20:1-12)
- Unapomtafuta na kumfuata Mungu, majaribu yanatokea
- Yehoshafati aliazimu kumwangalia Mungu kuliko kutazamia wenye mwili (20:1-3)
- Mfano mwema wa mfalme ulifuatwa na taifa zima (20:4)
- Mtu wa Mungu anafahamu, hakuna tengemeo lingine isipo Mungu pekee (Zaburi 46:1-7)
- Yehoshafati alimwomba Mungu – kwa ukuu wake (v) Mwaminifu (v.7) Mungu anayeaminika sana (v.8)
- “Macho yetu yakutazama ee Bwana” (v.12)
- Haijalishi shida zako – mtazame tu, tafuta usaidizi kutoka kwake pekee na utarajie kusaidiwa na yeye.
V. YEHOSHAFATI ALIJIBIWA MAOMBI YAKE (20:14-17)
- Roho wa Mungu alimjia Yahazieli mwana wa Zakaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeheli mwana Matania – mlawi wa wana wa Asafu
- “Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya Jeshi kubwa..kwa maana vita si vyenu, bali vya Mungu (v.15)
- Unapo mwamini Mungu kwa shida zako, vita si vyako tena, bali ni vya Bwana
- Mungu anachukua waajibu wa wote wanao jitwika shida zao kwake
- Wenye Imani kazi yao ni kusimama imara na kuuona wokovu wa Bwana (v.17)
- “Hatuta hitaji kupigana katika vita hivi”
VI. USHUHUDA WA YEHOSHAFATI (20:18-20)
- Yehoshafati aliinama na kuabudu Mungu
- Yehoshafati na ushuhuda wake “mwamini Bwana, Mungu wenu ndivyo mtakavyothibitika, waamini manabii wake, ndivyo mtakavyo fanikiwa” (v.20)
- Imani ndani ya Mungu inatuongoza kuwa wa Imani na manabii wake (Waebrania 6:12)
VII. SIFA NA IBADA (20:21-30)
- Imani inacheka juu ya mambo yasiowezekana na kusema “Itatendeka”. Yehoshafati alimwamini Mungu na kuamurisha sifa na ibada na nyimbo
- Waimbaji ndio walitangulia jeshi. Ahadi za Mungu ni kweli na Amina
- Huu ndio ushindi ushindao ulimwengu – Imani yetu
MWISHO
- Je, ni shida gani uliyenayo? Mwamini Mungu na nabii wake leo
- Je, adui zako wamekusanyika juu yako? Vita ni vyake Bwana.
- Je, una imani juu ya ahadi zake Bwana? Anza kuimba nyimbo za sifa na ibada. Adui amekufa, ni mauti milele.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025