Kings Of Judah Swahili Service

CHAGUO LA SULEMANI- BARAKA TELE

I WAFALME 3:1-15

UTANGULIZI

Hekima na moyo wa Adili haupatikani, lakini hupeanwa. Haupatikani duniani lakini huteremka kutoka mbinguni. Inasemekana kwamba Mungu alimpenda Sulemani (2 Samweli 12:24). Sasa inasemekana kwamba   Sulemani naye alimpenda Bwana (V.3).   Mungu anakupenda, hivyo nawe mpende Mungu wako. Sulemani mfalme alienda    Gibeoni kutoa sadaka mbele za Mungu. Akatoa sadaka Elfu kondoo. Sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu ile. Moyo wa Sulemani ulijaa mafikira ya utakatifu wa Mungu, umbaya wa dhambi na utakaso wa moyo. Sulemani alilala usiku huo akiona    unyonge wake na nguvu za Mungu. Usiku huo huo Mungu alimtokea Sulemani katika ndoto. Ndoto ni njia moja Mungu hunena na watu wake.

Hebu joo karibu tutazame:-

I.  MUNGU AKAMWAMBIA, OMBA UTAKALO NIKUPE (3:5)

  • Nani amesema omba utakalo?
  • Huyo ni Mungu muumba mbingu na inchi.
  • Huyo ni Mungu wa milele, Alfa na Omega.
  • Huyu ni Mungu mwenye nguvu na uweza.
  • Nafasi kama hii inatokea mara moja katika maisha na jibu lake linatosha wakati na milele.
  • Mungu alimpa Sulemani hudi wazi (Open Check)
  • Mungu ameweka neno hili mbele zetu zote (Waefeso 1:15-23)
  • Mungu alimtoa Mwanaye pekee kwetu

II.  UCHANGUZI BORA WA SULEMANI (3:9)

  • Nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili (Understanding heart)
  • Kila mtu anaposikia injili ya Kristo anapata fursa ya kuomba atakalo.
  • Sulemani aliomba moyo wa hekima, adili na ufahamu.

Huu ni uchaguzi Bora Maana:-

  1. Ombi lake lilijaza mahitaji yake yote (7-8)
  • Moyo wa adili, moyo wa kuongozwa na Bwana.
  • Moyo wa kuwaelewa watu na mioyo yao.
  1. Ombi lake lilimpendeza Mungu (v.10)
  • Maombi ya Sulemani haikuwa ya ubinafsi (Yakobo 4:3)
  • Maombi ya wengi wetu ni maombi ya ubinafsi.
  • Kumpendeza Mungu ni pamoja na kutembea naye (I Thesalonike 4:1-8)
  • Kumpendeza Mungu ni pamoja na utii (I Yohana 3:21-22, Mwanzo 5:24– Henoko)
  • Kuna mambo haimpendezi Mungu:-
  1. Kukosa Imani (Waebrania 11:6)
  2. Matendo ya mwili (Warumi 8:6-8)
  3. Kuwapendeza watu (Wagalatia 1:10)
  4. Dini isiyo na utakatifu wa ndani (Mika 6:8)

III. JIBU LA MUNGU KWA MFALME SULEMANI (3:12-13)

  1. Sulemani alipata aliyoomba (v.12)
  • “Tazama nimekupa moyo wa hekima na wa akili”
  1. Sulemani alipata zaidi ya maombi yake (v.13)
  • Nimekupa pia mali na fahari (Riches and honor)
  • Sulemani alitafuta kwanza ufalme wa Mbinguni, ndipo mengine yakaongezewa kwake.
  • Mfalme Sulemani alipata utajiri zaidi (I Wafalome 10:23)
  • Mfalme Sulemani alipata fahari mpaka leo (I Wafalme 10:24-28)
  • Mfalme Sulemani, ikiwa atamtii Bwana basi– siku nyingi (Waefeso 6:1-4)

 

MWISHO

  • Anayempata Yesu Kristo anapata moyo wa Adili, hekima, siku nyingi, afya, Amani, mali na furaha. (Mithali 3:13-16)
  • Mungu atupatie moyo wa adili, mali na fahari hili watu wa dunia wabarikiwe kupitia kwetu.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *