Series Swahili Service USHINDI WA IMANI

DANIELI MTU WA KUAZIMU

DANIELI 1:1-21

UTANGULIZI

Kitabu cha Danieli kimetupwa katika tundu la simba kama Danieli mwenyewe.Wengine wanakataa kitabu cha Danieli kwa sababu ya miujiza na unabii uliopo. Lakini Yesu Kristo alikitaja sana kitabu cha Danieli hivyo kukipatia kiti katika maadiko matakatifu. Sir Isaack Newton alisema, “ Ukristo umejengwa juu ya unabii wa Danieli”. Baada ya Yerusalemu kunusuriwa na mfalme wa Babeli mwaka wa 605 B.C. Danieli na wezake walishikwa mateka na kupelekwa Babeli, maili 800 hau Kilomita 1,200. Danieli alikuwa na umri wa miaka 14 wakati huo. Kitabu cha Danieli kina sehemu mbili (1) Maisha ya Danieli (1-6), (2) Maono ya Danieli (7-12). Katika Danieli twajifunza kwamba 1. Mungu yuko katika enzi na anaogoza dunia hii 2. lengo la maisha, 3. Kusubiri na kuvumilia 4. Uaminifu wa Mungu.

Hebu tuone:-

I.  TABIA YA DANIELI (1:3-5)

  • Hatujaelezwa juu ya wazazi wa Danieli lakini tunapotazama maisha na tabia yake, twaona mikono ya wazazi wema.
  • Utu wa Danieli na tabia yake inaonyesha kwamba kanuni za maisha na msingi kamilifu katika maisha ya utotoni na ujana.
  • Utu wa mtu unakuwa tayari kwa umri wa miaka 12.
  • Katika miaka ya kwanza ya maisha kunao mitego mingi.
  • Kumjua Kristo kibinafsi ndilo jambo la maana kabisa na zaidi katika maisha ya mjini.
  • Danieli alielewa sana na maandiko ya 2Timotheo 1:12
  • “Kwa maana namjua yeye niliyemwamini na kusadiki ya kwamba aweza kulinda kila nilichoweka amana kwake hata siku ile”
  • “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya Imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho (I Perto 1:5-9)

II. MAJARIBU YA DANIELI (Danieli 1:5-6)

  • Majaribu ni lazima yaje. Majaribu yanachagia sana kukua kwa Imani.
  • Amri ya mfalme ilikuwa wachanguliwe vijana wa uzao wa kifalme, vijana wasio na mawaa, wazuri na uso, wajuzi na hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu. Watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme (v.4)
  • Mafunzo katika “Royal College” ilichukua kipindi cha miaka mitatu.
  • Wafundishwe elimu ya Wakaldayo na lugha yao.
  • Wakaldayo walikuwa wanasiasa, wanaphilosophia, wanatheologia na waalimu wa taifa
  • Lakini pamoja na elimu– chakula chao kilikuwa chakula cha kifalme kilicho tolewa kwa sanamu na mingu ya babeli.
  • Dunia hii ina vyakula na vunywaji vyake (Ii Wakorintho 8:4-13)

III. AZIMIO YA DANIELI (Danieli 1:8)

“Lakini Danieli aliazima moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme wala divai aliyokunywa” (Warumi 14:21)

  • Lazima waliookoka kusimama kwa imani yao hata panapo misimamo ya waliowengi.
  • “Mchungwa unakaa mchungwa hata jangwani”
  • Danieli aliazima moyoni hatakula na kunywa divai-hatajitia unajisi.
  • Tunahitaji kuwa na mpango kamili na mpango wa ziada kuishi maisha ya utakatifu kila mahali (Basic and contigent plan) (Zauri 106:46, Isaya 43:2-5, I Wakorintho 10:13)

IV. DHAWABU YA DANIELI (Danieli 1:9-21)

  • Mungu alimpa Danieli kibali (v.9)
  • Danieli na wenzake walipandishwa cheo.
  • Mungu aliwapa afya kuliko wenzao.
  • Nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfale (V.15)
  • “Mtama pekee yake”- Nyama, divai na mapochopocho si kila jambo maishani “Mtama tu” na Yesus Kristo inatosha.
  • Uungu (godliness) ni faida kuu zaidi (I Timotheo 6:6-7)
  • Uungu (godliness) ni tabia ya juu zaidi na uhusiano juu zaidi kwa Mungu na mwanadamu.
  • Hekima iliyomfaidi Danieli haikupatikana katika shule za usomi, lakini katika uhusiano na ushirika na Mungu wa Mbinguni.

 

MWISHO

  • Azimia kutojua chochote mbele za wanadamu, isipokumfahamu Yesu Kristo na yeye kusulubiwa msalabani.
  • Hekima ya Mungu itakuwa yako, maarifa na ujuzi wa Mungu ndiyo nguvu juu ya nguvu za giza.
  • Leo pata kuokoka, jitoe kabisa kwake Bwana, pokea kibali chake leo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *