I SAMWELI 1:1-11
UTANGULIZI
Hanna ni picha nzuri ya mama na umama. Hana alitaka kuwa na watoto wake. Hana alimwomba Mungu mtoto na kumlea kwa kazi ya Mungu.
Elkana alikuwa kuhani hasiye mwaminifu kabisa, maana alikuwa na wake wawili.
Kuhani mkuu alikuwa Eli, naye alikuwa na wana wawili yaani; Hofni na Finehasi, wote wawili walikuwa waasi (I Samweli 2:12,17,29)
Imani ya Hana ilikuwa katika hali ngumu sana, Penina alikuwa mke mwenza mwenye chuki na matusi ya kila siku. Penina alifikiri kwamba Hanna alikuwa tasa, lakini kumbe Mungu alimfunga tumbo. Kuna watu wanafikiri wewe ni tasa, kumbe wakati wako ujafika !! Samweli twafahamu lakini watoto wa Penina. Penina alifikiri matusi yake yatamfanya hana kukata tamaa, kumbe yalimfanya Hana kuomba kwa Imani. Watu wanao kuchukia wanafanya Baraka za Mungu kutimia katika maisha yako.
Hebu Tuone:-
I. HATUA SABA ZA MAJIBU KWA MAOMBI.
Mahitaji makuu yanatuelekeza kwa maombi,
- a)Hana hakuwa na mtoto, “Mungu alikuwa amemfunga tumbo” (v.5)
- b)Hana alichukiwa sana na Penina, hivyo Penina humchokoza sana na kumsikitisha (v.6)
- c)Eli alikosa kumuelewa Hana-utakuwa mlevi mpaka lini? (v.14)
Mahitaji makuu yatufanya kuomba na kutoa sadaka.
- a)Kujitoa– Hana aliweka nadhiri (v.11)
- b)Hana alifunga Saumu (zaumu) (v.8)
- c)Hana alitoa wakati wake wa jamii kuomba Bwana (v.9)
- d)Hana aliomba sana na kulia sana (v.10)
Sadaka kuu inatufanya kuzidi katika maombi.
- A)Mwaka kwa mwaka—Jamii ya Elkana walienda maombi pale shilo (v.7)
- B)Kristo alisema omba nawe, utapewa, bisha nawe utafunguliwa, tafuta nawe utapata (Mathayo 7:7)
Imani kuu huzaliwa kutokana na mahitaji makuu, tamaa kuu na sadaka kuu (V.11)
- Hana kweli aliomba
- Hana alitoa nadhiri (Hesabu 6:1-21)
Imani kuu huleta majibu makuu.
- A)Eli alimwambia Hana- “Enenda kwa Amani, na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyo mwomba” (v.17)
- B)Mungu alimkumbuka Hana– Hana alishika mimba (V.19-20)
Majibu makuu lazima kufuatiliwa
- a)Jina la mtoto– Samweli—”Nime mwomba kwa Mungu”
- b)Hana alikaa nyumbani mpaka mtoto akue (V.22)
- c)Hana alimtoa huyo mtoto Samweli wakfu kwa Bwana (V.26-28)
Hana alifanya Ibada Kuu
- Hana aliomba na kuimba nyimbo za sifa (2:1)
- Hana alimwomba Bwana mtoto moja, Mungu alimpa watoto saba (2:5, Waefeso 3:20)
- Mungu huwalinda watu wake (2:9)
- Kwa nguvu zetu hakuna atakayeshinda.
- Washindanao na Bwana watapondwa kabisa.
MWISHO
- Imani lazima kuomba
- Je, umeokoka? Leo ndio wakati wa kuokoka.
- Je, penina wako yupo ?Ameshindwa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
