Swahili Service

HASIRA HAIFANYI MAPENZI YA MUNGU

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI

SOMO: 1 SAMWELI 25:1-44 (2-13).

 

Je, kuna mtu hapa ambaye hana shida ya hasira? Kula mmoja wetu anapata kuwa na hasira. Shida ya hasira ni kwamba kuidhibiti ni kitu kigumu sana. Hasira ni tawala katika maisha. Hasira ni kama moto, baadaye inazimika, lakini inaanza uaribifu mkubwa katika mapito yake.

Biblia inaongea sana juu ya hasira na jinsi ya kuidhibiti hasira kabla ya kuleta madhara yake.

  • Waefeso 4:26 “Muwe na hasira, ila msitende dhambi, jua lisichwe na uchungu wenu bado haijawatoka.”
  • Zaburi 37:8, “Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.”
  • Mithali 14:28, “Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi, bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.”
  • Mithali 19:11, “Busara ya mtu huiahirisha hasira yake, nayo ni fahari yake kusamehe makosa.”
  • Mhubiri 7:9, “Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kufuani mwa wapumbavu.”
  • Matthayo 5:22, “Basi mimi nawaambieni, kila amwoneaye ndugu yake hasira, itampasa hukumu, na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza, na mtu akimwapiza, itampasa jehanamu ya moto.

Leo twajifunza juu ya Daudi na hasira yake. Kila mmoja wetu atapata kujioji moyoni juu ya jambo hili la hasira na shida ambazo hasira imeleta katika maisha.

DAUDI NA HASIRA YAKE-1 Samweli 25:2-13; 21-22.

2-11 sababu ya hasira yake.

  • Daudi alikuwa katika ukimbizi kwa kuogopea maisha yake kutoka kwa mfalme Sauli.
  • Daudi pamoja na watu 400 ni wakimbizi kule jangwani.
  • Watu waliomjia Daudi jangwani ni watu wenye dhiki, wenye madeni na watu wenye uchungu mioyoni mwao.
  • Kazi zao mle jangwani ni kuwalinda wafugaji kutokana na wanyama na vita vya makabila-1 Samweli 23, 1 Sam. 25:7.
  • Kazi hii ndio iliwapa chakula Daudi na watu wake.
  • Baada ya kuwalinda hawa watu, Daudi aliwatuma watu wake kwa Nabali-25:5-12.
  • Lakini Nabali alikuwa mjeuri. Badala ya kuamkia salamu na barua ya heri kutoka kwa Daudi-Nabali alikashifu Daudi na watu wake.
  • Nabali alimtusi Daudi, akamwita muasi wa mfalme.
  • Daudi alikasirika sana, lakini hasira yake haikufanya mapenzi ya Mungu-“Hasira inaendesha kila kitu vibaya.”
  • Alexander the Great, hata ingawa alishinda vita duniani kote, lakini Alexander hakuweza kushinda hasira ya moyo wake.
  • Siku moja rafiki yake Alexander kwa jina Cletus, rafiki wake wa ujanani na jemedari katika jeshi la Alexander, alilewa pombe akamtusi Alexander, kwa hasira Alexander alitupa mkuki na kumuua Cletus papo hapo.
  • Usipodhibiti hasira yako, hasira yako itakudhibiti wewe.

Vitendo vya Daudi juu ya Nabali-V. 12-13.

  • Daudi alipopokea habari kutoka kwa wajumbe aliowatuma kwa Nabali-V. 12-13.
  • Daudi alipopokea ujumbe mbaya kutoka kwa Nabali, kwa hasira alichukua jeshi lake (600) wakaenda kwa Nabali.
  • Hasira itakufanya kuua watu (overkill)
  • Hasira itakufanya kufanya mambo maovu zaidi na ya ujinga.
  • Kwa kweli Nabali alikuwa mtu bila adabu na mwovu katika Matendo yake-1st Samweli 25:3.
  • Nabali alijifundisha tabia mbaya, hakuwa na heshima kwa watu. Hakujua jinsi ya kuishi na watu.
  • Maana ya jina Nabali ni “Mjinga.”
  • Lakini kwa hasira Daudi alikuwa mjinga zaidi, “Hasira ni ujinga.”

Matokeo ya hasira ya Daudi-V. 21-22.

  • Hasira inatufanya wajinga na wenda wazimu.
  • Hasira inatufanya kusema mambo yasio na msingi.
  • Hasira itakufanya mjinga.
  • “Mtu wa kiburi hana Mungu; mtu wa wivu hana rafiki wala jirani, lakini mtu wa hasira hana nafsi wala utu.”

HASIRA YA DAUDI ILIKABIDHIWA-25:14-31.

Abigaili alikuwa mwanamke mwenye busara-V. 14-20.

  • Nabali alikuwa mjinga lakini mkewe alikuwa mwanamke mwenye busara.
  • Maana ya jina Abigaili ni “Baba yangu ni furaha” (my father is joy).
  • Abigaili alikuwa mwanamke mrembo sana kwa umbo na mwanamke wa hekima.
  • Abigaili alikuwa mrembo na pia mwenye akili nyingi.
  • Abigaili aliposikia habari za mume wake na ujinga wake alichukua hatua ya haraka sana.
  • Abigaili alitayarisha chakula na vitu ambavyo Daudi alikuwa ametumana.
  • Abigaili alienda kumlaki Daudi akiwa na matumaini ya kubadilisha nia yake.
  • Abigaili alijaribu sana kumlinda mume wake-V. 14-17.
  • Nabali hakuwa mtu anaweza kuongea na mtu, alikuwa mtu jeuri (stubborn)
  • Ni kitu chema kusikiza mke. Mungu alipokupa hekima alimwaga nusu ya hio hekima katika mke wako!!
  • Mke anaitwa msaidizi (helpmeet)

Hekima ya Abigaili-V. 23-31.

  • Abigaili alipokutana na Daudi, alinyenyekea mbele zake.
  • Mara 16 abigaili anamwita Daudi “Bwana wangu”, mara 6 Abigaili alijiita “mtumishi.”
  • Abigaili alikubali Nabali mumewe ni mtu wa kiburi na mjinga-Vs. 25.
  • Abigaili aliomba msamaha juu ya mumewe Nabali-27-28.
  • Abigaili alimsihi Daudi asimuue Nabali-Yakobo 1:19-20.

Matokeo ya maombi ya Abigaili-V. 32.

  • Busara na hekima ya Abigailli ilipunguza hasira ya Daudi.

HASIRA YA DAUDI ILIPOESHWA-V. 32-42.

Daudi aliwacha hasira yake kwa sababu alifungua moyo wake kusikiza Abigaili-32-35.

  • Biblia inasema tusilipishe ubaya kwa ubaya-Warumi 12:17-21.
  • Mungu alimlipa Nabali, akamuua.

Hasira ya Daudi ilipoeshwa na Mungu mwenyewe-V. 36-42.

  • Abigaili aliporudi nyumbani alimkuta Nabali amelewa sana.
  • Nabili alikufa kwa mshtuko wa moyo (stroke).
  • Baada ya siku kumi Nabali alikufa.
  • Baadaye Daudi alipata kumuoa Abigaili akawa mke wake.
  • Hivyo tusiwache hasira kututawala maisha.
  • Tukamwache Mungu kulipisha kisasi.

MWISHO

  • Tunahitaji kuleta hasira zetu mbele za Bwana.
  • Je, umejaa hasira moyoni? Miaka mingapi katika hali ya hasira?
  • Kamwache Mungu akusaidie na hasira yako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “HASIRA HAIFANYI MAPENZI YA MUNGU”

Leave a Reply to Jack Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *