Swahili Service TIMOTHY

JIHADHARI USIANGAMIE KWA HABARI YA IMANI

I TIMOTHEO 1:18-20

UTANGULIZI

Mtume Paulo anamshauri Timotheo ajiadhari sana hasipate kuangamia katika habari ya Imani (Spiritual shipwreck). Hivyo Paulo anampa Timotheo hatua tano za kujilinda na kuangamia kiroho. Kumuishia Kristo katika ulimwengu huu si rahisi. Watu wengi wameangamia katika Bahari ya Imani. Katika mwaka wa 1912– Meli ya abiria iliyokuwa kubwa zaidi duniani iliangamia baharini. Meli hii illitwa RMS       Titanic. Meli hii ilibeba  abiria 2,228 siku hio 14/04/1912; wenye kuijenga meli hii walisema haitaweza kamwe kuaribika (Invincible) lakini siku hio meli iligonga mwamba baharini na   kuzama, watu 705 ndio walipona kifo, watu 1,523 walikufa maji.

Timotheo alikuwa mwanaye Paulo kiroho. Timotheo aliitwa kuwa askari mwaminifu wa Yesu Kristo, apigane vita vya Imani. Paulo anamweleza Timotheo maana yake kuwa  askari mwema wa Kristo. Maisha ya kuokoka ni ngumu zaidi, vita ni vikali na adui ni wengi (weafeso 6:12). Vita hivi huko juu zaidi ni dhidi ya Mungu na shetani. Malaika watakatifu na malaika-daimoni na mapepo. Tena ni vita kati yetu na pepo wambaya sana (Yuda 1:9) Vita vyetu ni tatu; majaribu ya adui na mitego, uadui wa dunia hii na vita vya dani juu ya mwili (Yohana 15:18) Watu kama Himenayo na     Iskanda (Hymenaeus and Alexander) walipotea katika bahari ya Imani. Himenayo aliangamia kwa kuacha ukweli wa neno la Mungu juu ya ufufuo– kiyama ya wafu (II Tim.2:17-19).    Iskanda alipinga sana neno la Mungu (II Tim.4:14-15)

 

Hebu tuone hatua tano za kujilinda na kuangamia kiroho:-

 I.  SHIKA SANA NENO LA MUNGU (V.18)

  • Paulo anamkabidhi Timotheo agizo– shika neno.
  • Yakobo 1:22-25– Kutenda Neno la Bwana.

II.  FIKA KIWANGO CHAKO (V.18)

  • Kulingana na jinsi neno la unabii yalitangulia juu yake (Fulfill your potential)
  • Usidharau kipawa kilicho dani yako (I Tim.4:14-16)

III. VIPIGE VILE VITA VIZURI (V.18)

  • Lengo letu ni nzuri, tunaye jemedari hodari, tuko na vifaa nzuri zaidi (Waefeso 6:10-18)

IV.  LINDA SANA IMANI (V.19)

  • Wacha Imani yako ikuongoze maishani
  • Imani dani ya Kristo ilimpa Timotheo Amani (Wafilipi 4:7)

V.  UWE MWAMINIFU (V.19)

  • Uwe na dhamiri njema. Dhamiri inatufundisha kwamba, tunapofahamu kweli na uongo, kufuata ukweli.
  • Himenayo na Iskanda walitolewa kwa shetani wafunzwe kutomtukana Mungu.

VI.  MATOKEO YA KUMWACHA MUNGU (V.20)

  1. Hawa wanaume wawili ;Himenayo na Iskanda walipeanwa kwa shetani, wafundishwe kutomtukana Mungu (Wakorintho 5:5)
  2. Hakuna mtu anaye fanya dhambi peke yake. Dhambi zetu zinawahusu watu wengine (wagalatia 6:9, Waebrania 12:6-12, I Johana 5:16, I Wakorintho 11:30.)
  3. Dhambi inakukosesha ushuuda na kukosa Imani mbele ya watu– jamii na washirika

 

 

MWISHO

  • Tarehe 14/04/1912 R.M.S Titanic, meli ya maana zaidi duniani, meli iliyetukuzwa sana , wengi waliona titanic itatumika miaka mingi na  kuwanufaisha wenyewe, lakini kwa makosa kidogo, titanic ilizama –Atlantic.
  • Je, maisha yako yanapotia kikomo watu watasemaje? (II Tim.4:7) “Nime vipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda”
  • Katika bahari ya maisha, majaribu ni mengi na mikosi, lakini Bwana yupamoja nawe, maliza safari vyema. Amen

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *