DANIELI 4:1-37
UTANGULIZI
Huu ni ushuhuda wa mfalme Nebukadneza. Alitoa ushuhuda huu kama ujumbe wa serikali yake rasmi (V.1) mtu anaweza kufahamu mengi sana ya njia za Mungu na mapenzi yake, lakini mtu huyu awe mbali sana na neema inayo okoa. Nebukadneza alikuwa mtu aliyekubalika sana na Mungu, pia alikuwa na nafasi kuu kuokoka. Mungu alimwonyesha Ishara kuu juu ya enzi za mataifa katika historia ya ulimwengu huu. Alisikia Danieli mtu wa Mungu akitafsiri ndoto zake, aliona jinsi Mungu aliwaokoa Shedraki, Meshaka na Abednego kutoka motoni, pia Nebukadneza alikuwa tayari kushuhudia ukuu wa Mungu (3:29). Mungu pia alimwonya Nebukadneza (4:14,16,27). Leo hii Mungu amenena kwa neema kupitia , ndoto, maono, onyo na upendo, lakini mwanadamu anakataa neema na nuru ya Mungu.
Hebu tuone:-
I. MFALME KATIKA NYUMBA YAKE (PALACE) V.4
- “Mimi mfalme nilikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikistawi katika nyumba yangu ya enzi”
- Alikuwa salama– alikuwa anastarehe katika nyumba yake.
- Nebukadneza alikuwa mfalme wa Babeli.
- Nebukadneza alikuwa tayari ameshinda Yuda na kuaribu Yerusalemu na kushika mateka Yuda.
- Nebukadneza alitawala miaka 43, enzi ya dunia yote.
- Alikuwa amefauli kabisa- “Nikistawi katika nyumba yangu”
- Ustawi wa Nebukadneza ulipana sana– Mashamba hewani na kuta pana zaidi kuzunguka mji wote.
- Alikuwa amejenga hekalu nyingi kwa miungu yake.
- Nebukadneza alikuwa shujaa hodari zaidi.
- Alitawala dunia yote.
II. MFALME JUU YA KITANDA NA PILO YAKE (4:5)
- Ndoto yake- “Niliona ndoto”
- Yakobo aliota ndoto (Mwanzo 28:10-22)
- Pharao aliota ndoto (Mwabzo 41:14-24)
- Nebukadneza aliota ndoto (Danieli 4:19-37)
- Yusufu, Petro, Mke wa Pilato waliota ndoto zao (Ayubu 33:14-18)
- Hofu ya ndoto yake- “Nilifadhaika sana”
- Amri ya mfalme- “Akawaita– waganga, wachawi, wakaldayo na wanajimu”
- Danieli anakuja baadaye.
III. MFALME KATIKA UNABII (4:20-27)
- Kung’olewa kwake– mfalme atashushwa chini.
- Kufanywa ng’ombe (Mnyama) (v.25)
- Makao yake– pamoja na wanyama kondeni.
- Muda wake– Miaka saba.
IV. MFALME NA KIBURI CHAKE (4:30)
- Mfalme alipewa neema (v.27) Mika 6:8
- Uvumilifu wa Neema (v.29)- Miezi 12– mwaka
- Kina cha neema (v.30)
V. MFALME KWA NYASI (4:31)
- ilikuwa kwa ghafla
- Sauti ilitoka mbinguni.
- Sauti ilikuwa kwa mfalme pekee.
- Ilikuwa ngumu zaidi- “Ufalme umeondoka”
VI. MFALME KATIKA SIFA ZAKE (4:34-37)
- Nebukadneza aliyainua macho yake kuelekea mbinguni (34)
- Kila goti litapigwa (v.34), Wafilipi 2:10
- Nebukadneza alijirudi (v.36)
- Sifa zake kwa Mungu (v.37)
MWISHO
- Mwana mpotevu alizingatia katika moyo wake.
- Nebukadneza alijirudia.
- Kiburi ni dhambi mbaya sana, inawakosesha wengi mbingu na uzima wa milele (I Petro 2:25)
- Mbingu ndiyo inayetawala, nyenyekea mbele za Mungu (Kumbukumbu 8:10-18)
- Je umeokoka kweli? Nyenyekea na kuokoka leo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
