DANIELI 2:1-20
UTANGULIZI
Dani ya Danieli palikuwa na roho ya ufahamu, maarifa na hekima. Ufahamu, maarifa na hekima vinahitajika kukusaidia kupanda mpaka juu zaidi. “Kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga” (Luka 21:15) Danieli 1:8-9. Mungu anaweza kukupa ufahamu, maarifa na hekima, adui na marafiki wako hawataweza kushindana nawe, katika jina la Yesu Kristo. Tunahitaji kuomba ili Mingu atupe roho ya ufahamu, maarifa na hekima. Kushinda umaskini tunahitaji roho ya ufahamu, maarifa na hekima. Mungu wa Danieli ni yeye yule jana leo na milele. Upako wa ufahamu, maarifa na hekima ni wako leo. Mungu wa Danieli ni yule twamuona katika Danieli 1:17. “Mungu wa Danieli aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima. Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote na ndoto”. Mungu wa Danieli anawafunulia watoto wake katika ndoto na ufunuo.
Hebu tuone:-
I. MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA UFUNUO (Danieli 1:17)
- Huyu Mungu wa Danieli anaweza kukufunulia mtihani na siri zote.
- Shida yetu ni badala ya ndoto za kimbinguni, wakristo wengi wanaota ndoto za kufukuzwa na mashetani, mume na wake za kiroho.
- Mungu wa Danieli anaweka mbali ndoto na maono ya dhambi na kutishwa na wafu na mauti.
- Wakati mwingine tunakosa sana kuwaeleza watu ndoto na mipingo ya maisha yetu. Kukaa kimya mbele za Mungu na watu.
- Si kila mtu anakutakia mema, si kila mtu anapenda watoto wako wakiendelea.
- Tunahitaji hekima ya kunyamaza mbele ya Mungu na watu (Yohana 15:15)
- Kufichua siri zako mbele ya adui zako ni hatari kuu.
- Yusufu alifichua siri na ndoto zake kwa maadui zake.
- Tunahitaji maono na ndoto za kiungu tutekeleza maisha yetu.
II. MUNGU WA DANIELI NI MWENYE UWEZO MKUU (Danieli 2:21)
- “Yeye hubadili majira na nyakati; huzuru wafalme na kuwamilikisha wafalme, huwapa hekima wenye hekima, huwapa wenye ufahamu maarifa” (Dan.2:21)
- Mungu wa Danieli anatawala mataifa, tena hushusha wafalme.
- Mungu wa Danieli huwapiga wenye kiburi. Mungu wa Danieli huwaondoa wanaopiga watoto wa Mungu na kuwapa kupenya kwao (Breakthrough)
III. MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA SIRI NYINGI (Dan.2:22)
- “Yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri, huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake” (2:22)
- Mungu wa Danieli hufunua mambo ya siri.
- Siri zote za dunia na mbinguni anafahamu.
- Siri ya moyo wako na siri za watu wote anajua kabisa.
- Mambo yote ya jana, leo na milele Mungu anayajua.
- Hatima ya inchi na watu wake Mungu anajua.
- Mipango ya adui zako juu ya maisha yako Mungu atakujulisha.
- Mipango ya wachawi juu yako Mungu anakuonyesha ili upate kuomba na kuivunja.
- Ni vizuri kwako kufahamu siri ya Mungu juu ya maisha yako.
- Kuna siri ya Mungu kuhusu maisha yako, Biashara yako, kilimo chako, watoto wako, hekima ya Mungu inahitajika sana.
- Kuna siri katika kazi yako na maarifa yake.
IV. MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA UKOMBOZI (6:20-22)
- Danieli mara alitupwa katika tundu la simba, simba waliona mwana wa simba wa Yuda. Simba hawali simba!!
- Wanao mwamini Mungu wa Danieli wanajali sana kuomba na kufuchuliwa mpango wa Mungu siku baada ya siku.
V. MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU (6:26-27)
- Mungu wa Danieli ni yeye yule jana, leo na milele.
- Ikiwa umemwamini Mungu wa Danieli, basi tarajia ishara, maajabu na miujiza yake.
- Leo Mungu wa Danieli yupo hapa. Pepo wanao kusumbua lazima wakuache leo. Uponyaji wa Mungu wa Danieli ni wako leo.
- Mishale iliyotumwa kwako lazima kuwarudia waliotuma kwako.
- Nguvu za Mungu zitaanguka kwako leo
MWISHO– OMBA;
- Mungu wa Danieli inuka na kukimbiza wanao nikimbiza– katika Jina La Yesu Kristo.
- Kila nguvu za giza na uchawi zinazo tafuta uso wangu– kufa sasa katika jina la Yesu Kristo
- Kila uchawi uliopandwa katika mwili wangu,ng’olewa sasa katika Jina La Yesu Kristo.
- Nina funga kila kazi isiyo na faida katika maisha yangu katika Jina La Yesu Kristo.
- Kila roho ya mauti na jihanamu juu yangu toweka sasa katika Jina la Yesu Kristo.
- Mungu wa Danieli pita katika maisha yangu kwa ishara na maajabu. Nipe upako wa kibali katika jina la Yesu Kristo.
- Kila uchawi kutoka upande wa baba, mama na uchawi wa nyumba yetu, kufa sasa katika jina la Kristo.
- Roho ya nyoka na inge katika mwili wangu rudi kwa waliokutuma—Katika Jina La Yesu Kristo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
