MFULULIZO: MAPAMBANO YANAOBADILISHA HATIMA.
SOMO: KUTOKA 3:1-12.
Mapambano ya kweli na Mungu yanaamsha sababu ya Mungu kuishi, kunaleta ujasiri takatifu na agizo kwa muumini kutumika katika ufalme wa Mungu.
“Bwana alipoona yakuwa amegeuka ili atazame Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema Musa Musa, akasema mimi hapa”-Kutoka 3:4.
Mungu anadhihirisha kwa njia ajabu ajabu na kwa wakati tusipotarajia. Musa hakuwa katika maombi wala hakuwa katika ikulu Mungu alipomtokea. Musa alikuwa katika harakati za kuchunga kondoo za mkwewe mle nyikani baada ya kukaa katika maficho miaka arubaini (40).
Ni katika hayo maficho Mungu alimtokea Musa kupitia kijiti kilichowaka moto bila kuteketea.
Mapambano haya katika kijiti kilichowaka bila kuteketea, hapo ndipo maisha ya Musa ilibadilika kabisa. Hapa mbele ya Musa alijaribu kuwaokoa wana wa Israeli kwa nguvu zake binafsi lakini akaangukia patupu. Sasa baada ya miaka 40 ya unyenyekevu na kuwekwa tayari na Mungu, Mungu alimwita Musa kukamilisha mradi wa kuwaokoa wana wa Israeli lakini kwa nguvu na uwezo wa Mungu.
Kila mkristo wa kweli anahitaji mapambano katika “kijiti kinachowaka bila kuteketea.” Ni mbele ya uwepo wa Mungu tunapata kuelewa sababu yetu kuishi. Hofu inamalizika, udhuru nao inatoweka na watu wa kawaida wanakuwa mashujaa. Mungu angali anawaita watu, waume kwa wanawake leo, anawaita kutimiza agizo kuu. Hebu tutazame:-
MUNGU ANAJIDHIHIRISHA KWA WALE WAMTAFUTAO.
- Mapambano na Mungu yanaanza Mungu anapojidhihirisha kwa mioyo inayomfuata.
- Wale wanaopenda kumfahamu zaidi ni lazima wawe tayari kutambua sauti yake na kuitikia mwito wake kwao.
- Mungu anaongea kwa njia tofauti tofauti-Kutoka 3:2.
- Kijiti kinachowaka bila kuteketea kilikuwa ajabu kuu kwa Musa.
- Mungu anaweza kuongea kwa njia tofauti tofauti na za ajabu ili apate umakini wetu na kuwasilisha mapenzi yake kwetu.
- Kuwa katika kutarajia kiroho kunafungua njia ya Mungu kujivua kwetu-Kutoka 3:3-4.
- Mungu alipoona kwamba Musa amegeuka na kutazama kile kijiti kilichowaka bila kuteketea, alijua kwamba Musa amejiweka katika hali ya kupokea Ufunuo kubwa zaidi.
- Mungu anawaita watu kibinafsi na moja kwa moja-Kutoka 3:4.
- Mungu alimwita Musa kwa jina lake tena mara mbili!!
- Uhusiano wa Mungu na watoto wake ni wa kibinafsi.
- Mungu angali anawaita watu leo-Yohana 10:27.
- “Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.”
- Wakristo lazima wawe makini sana kuisikia sauti ya Mungu na kupokea mwongozo wake.
- Samweli hakujua sauti ya Mungu baadaye alipotambua alisema “Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia”-1 Samweli 3:1-10 (9).
MAPAMBANO NA MUNGU YANAHITAJI HESHIMA NA UTAKATIFU.
- Mungu ni mwenye upendo na rehema, lakini pia Mungu ni mtakatifu.
- Kila pambano na Mungu inatufundisha heshima, unyenyekevu na hamu ya kuishi watakatifu mbele za Mungu.
- Tambua utakatifu wa Mungu-Kutoka 3:5.
- Mungu alimwamuru Musa kuvua viatu vyake, kwa sababu alikuwa amesimama juu ya mahali patakatifu.
- Uwepo wa Mungu unadai heshima na utakatifu.
- Mkaribie Mungu kwa unyenyekevu-Yakobo 4:10.
- Kiburi ndicho kinavunja ushirika na Mungu, lakini unyenyekevu unafungua mlango wa ushirika mkuu na Mungu.
- Jitenge na dhambi-1 Petro 1:15-16.
- Mungu anatuita kuiga utakatifu wake katika kila eneo la maisha yetu.
- Mwabudu Mungu wako katika heshima na unyenyekevu wote-Waebrania 12:28-29.
- Ibada ya kweli inaanza kutoka kwa roho. Moyo unatambu Mungu ndiye mkuu na mtakatifu.
- Isaya alipopambana na Mungu alitambua dhambi zake kabla ya kupokea utakaso na agizo-Isaya 6:1-8.
MUNGU ANAWAITA WATU WA KAWAIDA KWA KAZI ISIYO KAWAIDA.
- Mungu hawaiti watu kwa sababu ya masomo yao ya juu au kwa sababu wameitimu-lakini Mungu anawapa hekima na ujuzi wale anaowaita.
- Mungu anawaita watu, anawakamilisha kwa neema na nguvu zake.
- Mungu anaona zaidi juu ya maisha yetu ya kale-Kutoka 3:10.
- Hata ingawa Musa aliona udhaifu wake, Mungu naye aliona mkombozi wa Israeli.
- Usidhubutu kuacha hofu kuwa kikomo na kidhibiti kwako-Kutoka 4:10-12.
- Musa aliona kwamba hana ujuzi wa kuongoea-Mungu alim’hakikishia kwamba atakuwa pamoja na kinywa chake na kumfundisha jinsi ya kunena.
- Mungu anatupatia kila tunachohitaji kwa kazi yake-Wafilipi 4:19.
- Mungu anapowaita watu anawapa chochote kinachohitajika kufanya ile kazi.
MAPAMBANO NA MUNGU YANATUPA AGIZO YA HUDUMA.
- Kila pambano na Mungu linaleta agizo la Mungu kwetu.
- Mungu anajifunua kwetu hili tupate kuwa vyombo kwa kazi yake.
- Mungu anawatuma wale anaowaita-Kutoka 3:10.
- Musa alitumwa kukabidhi farao na kukomboa Israeli.
- Tegemea uwepo wa Mungu-Kutoka 3:12.
- Hakikisho kubwa ya Mungu kwa Musa ilikuwa uwepo wake.
- Uwe mkombozi kwa wengine-2 Wakorintho 1:3-4.
- Wote wanaopokea neema ya Mungu, wameitwa kuleta tumaini na uhuru kwa wengine.
- Uwe mwaminifu mpaka mwisho-1 Wakorintho 4:2.
- Yesu Kristo aliwapa mitume wake agizo kuu-kupeleka Injili duniani kote-Mathayo 28:18-20.
MWISHO
- Pambano la Mungu na Musa latufundisha Mungu anajifunua kwa watu wa kawaida.
- Mungu angali anawaita watu hivi leo. Ametuita kama mabalozi wake duniani.
- Kama leo utasikia sauti yake na kuitii kwa unyenyekevu na imani, basi Mungu atakufanya chombo na mtume kwa kazi yake.
- Ikiwa utaitika, Mungu atakupa ushuhuda wa nguvu na kutimiza hatima yako aliyokupangia.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUSA MBELE YA KIJITI KILICHOWAKA MOTO. - October 18, 2026
- DISCOVERING GOD’S PURPOSE FOR YOUR LIFE - October 18, 2026
- FAITH IN THE FACE OF CHALLENGES - October 14, 2026
