UTANGULIZI
Kwa Wayahudi Musa ndiye mtu mwenye heshima kuliko wote katika historia yao. (Kumbu Kumbu 34:10-12). Kwa Israeli wote Musa ndiye Nabii mkuu, mwanasheria mkuu na mwana historia. Aliandika vitabu tano vya kwanza vya Biblia. Musa ndiye mtakatifu zaidi ya wote. (Hesabu 12:3). Musa aliwakomboa wana wa Israeli kutoka utumwa wa miaka 400 Misri. Musa aliishi kwa Imani. Njia ya Mungu ni njia ya Imani.
Hebu tuone:-
I. KWANZA, MUSA ALIKUWA NA URITHI WA IMANI. (Waeb. 11:23-24)
- Imani ya Musa alianza na wazazi wake.
- Wazazi wake waliona Musa ni mtoto mzuri yaani special.
- Wazazi waliona kwamba mtoto Musa hakuwa mtoto kawaida.
- Kila mzazi anaona mtoto wake ndiye mrembo zaidi, hata ingawa uso wake unaweza kupendwa na mama yake pekee.
- Amri ya Farao ilikuwa watoto wauliwe, idadi ya wana Israeli ilikuwa juu zaidi.
- Amramu na Yokebedi wazazi wake Musa walikuwa wa Imani, wakamficha mtoto Musa kwa miezi ya kwanza mitatu.(Kutoka 6:20)
- Imani haingopi hatari. Imani hufukuza hofu.
- Baada ya miezi mitatu, Musa alichukuliwa na Binti Farao, Imani huachilia jambo mikononi mwa Mungu.
II. PILI, MUSA ALIKUWA NA IMANI YA KUCHAGUA (11:24-26)
- Musa Alikataa– kuitwa mwana wa binti Farao. (v.24)
- Musa Alichangua– Afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha (v.25)
- Musa Alihesabu– Kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri. Alitazamia malipo.
- Musa aliweka mambo yote katika mizani
- Musa alikuwa amesoma elimu yote Misri. (Matendo 7:22)
- Chuo alichosomea Musa kiliitwa “The Temple of the sun” University. Chuo hiki kilikuwa “Oxford ya dunia ya kale”
- Musa alisoma, science, historia, Geographia, Dawa, nyota, kemia, philosophia, uchoraji, uimbaji na masomo yote ya jamii.
- Musa alisoma masomo ya vita, alikuwa miaka 30 alikuwa tayari jemedari wa vita. Alishida vita ya Misri na Ethiopia.
- Lakini Musa alichangua Yesu Kristo na wokovu kamili.
- Musa aliona dhambi na fahari zake ni kwa kitambo tu.
- Musa aliona afadhali utajiri wa Mungu, kuliko anasa.
III. TATU. MUSA ALISTAHIMILI WAKATI HASIPOONA KWA MACHO
- Musa aliacha Misri, alitoka kabisa
- Petro, Yakobo na Yohana waliacha nyavu zao zote (Luka 5:11)
IV. NNE, MUSA ALIMTENGEMEA MUNGU WAKATI ASIPO ELEWA (11:28)
- Musa alipotoka Misri baada ya ukombozi aliendelea Pasaka na kunyunyiza damu.
- Musa aliishi chini ya damu ya Mwana Kondoo
V. TANO, MUSA ALIKUWA NA IMANI YA KISIMAMA KATIKA BAHARI MUNGU AFANYE KAZI YAKE. (11:29, Kutoka 14)
- Musa aliwaambia Israeli “Simameni Imara” muone wokovu wa Mungu. (Kutoka 14:13-16)
- Kwa Imani Mungu aliwapigania Israeli (Kutoka 14:21-22)
MWISHO
¨ Imani ya kweli husimana imara katika dhoruba
¨ Imani ya kweli, hukataa, huchangua huhesabu
¨ Je, Imani yako imetenda nini?
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
