DANIELI 7 :28
UTANGULIZI
“Huu ndio mwisho wa jambo lile” (v.28) Yanayo tajwa hapa ni unabii wa mambo na hali ya mambo katika dunia hii. Kitabu cha Danieli kina sehemu mbili. Mlango 1-7 ni hadithi ya dunia, 7-12 ni upambanuzi wa ule unabii. Danieli kama mtu wa maono na ndoto alikuwa pia mtu wa vitendo. Hivyo maono ya Mungu ni lazima kutekelezwa.
Hebu tuone:
I. MAONO YA DANIELI (7:1-4)
- Maono haya, ufunuo na tafsiri zake ni marudio ya Danieli 2, sanamu aliyeona mfalme Nebukadneza yana fanana na hao “wanyama” wane wanao onekana katika Danieli 7.
- Kama jinsi jiwe lilikatwa mbila mikono na kulivunja ile sanamu vipande vipande, falme za dunia hii hapa “Mwana wa Adamu” atachukua mamlaka kutoka kwa wanyama hao (v.12-14)
- Ufalme wa serikali za mataifa ni kama “wanayama wa kali” mataifa yanatoka kwa “bahari kubwa” ya wanadamu (The sea of humanity)
- Hawa wanyama wote ni wanyama wanaokula nyama. (Beasts of prey)- wakadiri, wanao nyanyasa, wakali wanao kula watu wake, wafisadi!!
- Nguvu za hawa wanyama wa kali– ni nguvu zisizo eleweka (brute force)
- Serikali zao zinanyanyasa watu na kuwatawala kwa ukali wa upanga na bunduki.
- Mungu ameruhusu falme na mamlaka ya mwanadamu kwa kusudi lake mwenyewe.
- Tazama jinsi Kenya inaendelea pamoja na county goverments, ufisadi, ukoloni na wizi wa juu.
- Maono ya Danieli tayari yametimia pakubwa.
- Babeli, wamedina, waajemi, wagiriki na warumi falme zao tayari zimekuja na kuondoka.
- Falme zilizo duniani sasa nazo zitapita pia.
II. MWISHO WA STORI (7:28)
- Ufalme mpya unakuja– Helelujah!
- Histpria ya falme za dunia hii zimeandikwa kwa machazi na damu.
- Ufalme mpya utakuwa wa Yesu Kristo na watakatifu wake!
- Hebu tuone jinsi ufalme wa Mungu na Masihi wake utakuja;
- Kurudi kwa Mwana wa Adamu- (V.13) “Tazama mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu” ( Watakatifu)
- Huyu ndiye mfalme na kichwa cha mwanadamu.
- Wanyama wale walitoka duniani na baharini– lakini huyu ni Bwana wa Mbinguni (Mathayo 24:27)
- Kuvunjwa kwa ufalme na nguvu za wanyama– “Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyanganywa mamlaka yao” (V.12)
- Hawa wanyama wametawala miaka nyingi sana– lakini dunia haijamfahamu Mungu chini ya wanyama.
- Kwa ufalme na utawala wa wanyama ni ngumu kumfahamu Mungu wa Mbinguni!!
- Lakini “Mwana wa Adamu” Yesu Kristo anapotawala– ni haki yake kutawala na kumiliki– ulimwengu wote utafahamu Mungu.
- Ufalme mpya utatawazwa Duniani; “Naye akapewa mamlaka na utukufu na ufalme, ili watu wote wa kabila zote na taifa zote na lugha zote wamtumikie (v.14)
- Ufalme huu utakuwa wa dunia yote– watu wote, taifa zote na lugha zote.
- Mamlaka yake ni mamlaka ya milele– uflame usio weza kuangamizwa (v.14)
- Ushindi wa watakatifu “Nao watakatifu wake aliye juu wakapewa hukumu na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme” v.22
- Mwisho wa stori– Ni mwema sana kwetu(V.18)
- Watakatifu ndio watamiliki sio madhehebu na dini waliokombolewa (I Wakorintho 6:2)
- Wakati mwema unakuja kwa watakatifu– mwenye kumtengemea, kumtumikia, wanaoteseka kwa kazi ya Mfalme.
- Wanao penda dhambi hawatakuwako kwa maana ufalme wa Mungu sikula na kunywa, lakini ni Haki, Amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
MWISHO
- “Mwisho wa Stori” utakuwa upande gani wewe?
- Watakatifu wa Aliye juu watatawala na kumiliki milele na milele.
- Wamebarikiwa walio ndani ya Kristo Yesu.
- Je, umeokoka, leo ni siku ya kuokoka.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
