Swahili Service

NEEMA YA KUOKOKA

MFULULIZO: NEEM YA MUNGU.

SOMO: WAEFESO 2:8-9.

 

Neema ya kuokoka ni neema ya Mungu inayokoa mtu kutoka dhambini, hukumu, mauti ya kiroho na kutengana na Mungu milele. Neema ya kuokoka inamleta mtu wokovu kupitia Imani ndani ya Yesu Kristo.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya Imani ambayo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu”-Waefeso 2:8-9.

Neno neema (charis) inatufundisha kwamba wokovu si kitu tunaweza kununua, kufanyia kazi au kufikia juhudi za mwanadamu, bali wokovu ni kibali cha Mungu kwa mwanadamu asiyestahili.

  • Mtu anaweza kuwa mtu mwema sana, bado anahitaji wokovu.
  • Mtu anaweza kuwa mtu wa dini sana, bado anahitaji kuokoka.
  • Mtu anaweza kuwa wa kanisa sana, bado anahitaji kuokoka.
  • Mtu anaweza kuwa Tajiri, msomi, mashuhuri, mheshimiwa, mrembo, sifa na cheo cha juu zaidi, bado anahitaji kuokoka, anahitaji neema ya kuokoka.

Mahitaji makuu ya mwanadamu sio fedha, maendeleo, elimu, afya na utawala mwema, mahitaji makuu ya mwanadamu ni wokovu!!

Mungu alimtuma mwana wake duniani kuokoa wenye dhambi-Yohana 3:16-17.

  • Neema ya kuokoa ndio neema ya juu zaidi.
  • Neema ni mtu-yaani Yesu Kristo-Tito 2:11-14. Hebu tutazame:-

NEEMA YA KUOKOA INAFUNUA KWAMBA HATUWEZI KUJIOKOA-Waefeso 2:8-9.

  • Mtume Paulo anaeleza kwamba wokovu si kazi ya mwanadamu.
  • Mwanadamu anapenda sana kujitatulia shida zake kwa nguvu zake mwenyewe.
  • Tunasema- “Nitajibadili, nitakuwa mwema zaidi, nitafanya vizuri zaidi, nitasahisha maisha ya kale, nitajirudisha kwa Mungu” lakini dhambi ina nguvu zaidi kuliko tabia ya mwanadamu.
  • Tunahitaji wokovu. Neema ya kuokoa inakuja kwa mtu yule anatambua “Mimi ninahitaji Mungu.” Huu ndio mwanzo wa kuokoka.

NEEMA YA KUOKOA INATUPATA KATIKA HALI YA DHAMBI-Warumi 5:8.

  • “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi-Warumi 5:8.
  • Ni wakati tuliokuwa wenye dhambi Kristo alitufia msalabani.
  • Mungu hakutungoja tuwe wema apate kutuokoa na kutupenda bali ni wakati tulikuwa wenye dhambi.
  • Tunamjia Kristo jinsi tulivyo, yaani wenye dhambi.

NEEMA YA KUOKOA NI KUPITIA KWA YESU KRISTO-Yohana 14:6.

  • Wokovu wa kikristo ni ndani ya Yesu Kristo pekee.
  • Yesu Kristo ndiye njia pekee ya kuokoka-Matendo 4:12.
  • Pale msalabani Yesu Kristo alibeba kile mwanadamu angaliweza kubeba.
  • Ujumbe wa neema si kwamba dhambi haina maana na uzito, lakini ni zito kiasi Yesu Kristo akalipa gharama yake pale msalabani.
  • Msalaba unaonyesha mambo mawili-
  1. Uzito wa dhambi-“Golgotha”
  2. Ukuu wa upendo wa Mungu kwetu, “Kalvari.”

NEEMA YA KUOKOA INASAMEHE DHAMBI ZA KALE-2 Wakorintho 5:17.

  • Jambo kuu ya wokovu ni msamaha wa dhambi.
  • Kuna watu wengi wanaoishi maisha yao ya asili kwa wakati uliopo, lakini katika nafsi na hisia zao wanaishi wakati uliopita, wanaishi wakikumbuka:-
  1. Makosa yao, upungufu wao, dhambi zao za kale, maamuzi yao mbovu, kusononeka kwao, aibu yao, shida za mausiano yao ya jamii, ndoa na urafiki.
  • Wanajuta sana mambo ya kale, lakini mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo ni kiumbe kipya, ya kale yanapita mapya yanakuja.
  • Neema inasema “Mambo ya kale ni historia ya maisha yako, lakini ya kale sio mwisho wa hadithi yako.”
  • Petro alimkana Kristo lakini alipata urejesho, Paulo alitesa kanisa lakini alibadilika na kuwa mtume wa Yesu Kristo. Mwanamke msamaria alikuwa na historia mbaya, lakini alibadilishwa na kuwa muinjilisti.

NEEMA YA KUOKOA INATUWEKA HURU KUTOKA HUKUMU-Warumi 8:11.

“Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”

  • Neema inakuelekeza sana esu Kristo na kusema, “Ona yale Yesu Kristo amekutendea.”
  • Hii si kusema dhambi si mbaya, lakini neema inatuonyesha uhusiano mpya na Mungu mahali toba, msamaha na maisha mapya yanawezekana.

NEEMA YA KUOKOA INASAMEHE, INABADILISHA NA KUTUPA KITAMBULISHO MPYA-Tito 2:11-12.

  • Neema ya kuokoa inabadilisha tamaa zetu, dhamana zetu (values) nia zetu, mahusiano yetu, misemo yetu, maamuzi na uhusiano wetu na Mungu.
  • Mbele ya kuokoka mtu anaweza kujitambulisha kama “mimi bure, sijapata kufaulu, nimekaliwa na watu na Mungu, hakuna mtu anayenipenda.”
  • Lakini wewe sio wa kale, sasa ndani ya Yesu Kristo na waokovu wake wewe ni “mtoto wa Mungu, umesamehewa dhambi, kiumbe kipya, umekombolewa umepatanishwa na Mungu.
  • Kitambulisho chako hakitegemei mambo yaliyotendeka juu ya maisha yako.
  • Kitambulisho chako kinaunganika na yale Yesu Kristo amekutendea.

NEEMA YA KUOKOA INAWAFIKIA WOTE, HATA WALE WAMEACHWA NA WAPENZI WAO-Warumi 3:23.

  • Neema ya kuokoa ni ya maana kwa sababu kila mtu amefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Hakuna mtu anaweza kujisifu mbele za Mungu.
  • Waliosoma na wajinga, masikini na Tajiri, mhubiri na mshirika, kiongozi na mtu wa kawaida wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
  • Wote wanahitaji Yesu Kristo na neema yake. Kwa msalaba wa Kristo watu wote wanatoshana, wote ni waombaji masikini, wote wanaomba rehema za Mungu.
  • Wakati mwingi umma na jamii inawatupa watu na kusema, “Hakuna tumaini kwake.”
  • Marafiki huenda wakasema “Huyu hawezi kubadilika.” Wengine wanasema “huyu ni bure.”
  • Lakini hakuna hali iliyo ya kudumu.
  • Mtu unayemkataa na kumtupa anaweza akawa ushuhuda panapo neema ya kuokoka.

NEEMA YA KUOKOA SIO LESENI YA KUFANYA DHAMBI-Warumi 6:1-2.

  • Tunapofundisha neema, ni lazima pia kuleta mizani. Watu wengine wanaelewa ovyo juu ya neema, wanasema, “Kwa maana Mungu amenisamehe dhambi zote, kwa sababu Mungu hawezi kuniacha, basi nitakaa ndani ya dhambi.”
  • Lakini mtume Paulo amekataa mafikira hayo-Warumi 6:1-2.
  • Neema ya Mungu haikubali kuishi katika dhambi. Neema inaleta utakatifu na inatufundisha kukataa dhambi zote-Tito 2:11-12.

NEEMA YA KUOKOA INAWAPA TUMAINI WALIOVUNJIKA MIOYO NA KUWAFANYA WATU WA SHUKRANI.

  • Kuna watu wanaocheka nje, lakini ndani yao wanahukumiwa, aibu, hofu, kusononeka, ni watupu ndani yao. 
  • Neema ya kuokoa inanena inawaambia “Mungu hajakuacha.”
  • Neema ya kuokoa inawaambia waliohukumiwa “kuna msamaha mbele za Mungu.” Neema inawaambia walioanguka “Rudi kwa Mungu wako.” Kwa waliopotea “Kuna njia ya kurudi nyumbani.”
  • Neema ya kuokoa inazaa ndani yetu shukrani na sifa.
  • Neema ya kuokoa inasema “Asante Bwana kwa yale umetenda kwangu-1 Wakorintho 15:10.

MWISHO.

  • Neema ya kuokoa imo hape leo, neema hii inakuita leo.
  • Kama bado kuokoa-leo kunao msamaha wa dhambi kwako, uje sasa.
  • Kama umeanguka-inuka rudi kwa Mungu wako.
  • Kama umepotea-kuna njia ya kurudi nyumbani.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *