Swahili Service

RUDI BETHELI.

MFULULIZO: YAKOBO; ALIFANYA MIEREKA NA MUNGU.

SOMO: MWANZO 35:1-29; 2 TIMOTHEO 2:13

 

Mrudie Mungu, acha Mngu akakuhudumie na akupe nguvu za kupigana na yote yaliyo mbele zako.

Kuna methali ya kiafrika inayosema- “Mtu anaye jaribu kutembea na njia mbili safari moja atararua suruali yake.”

Hivi ndivyo ilivyo tunapotaka kumtumikia Mungu na pia kuitumikia dunia hii. Watu wa namna hii wanajaribu sana kutotembea na Mungu na pia kuyaishi maisha ya dunia hii safari moja. Hivi ndivyo Yakobo alivyo ishi maisha yake mpaka aliporudi Betheli.

Mungu alimwita kurudi mpaka Betheli, lakini Yakobo aliamua kuishi mle Shekemu maili 15 (25km) kutoka Betheli. Yakobo alipenda Shekemu kwa sababu Shekemu palikuwa mahali pa makutano ya njia kuu. Palikuwa mahali pa biashara nyingi. Hapo Yakobo angeweza kupata utajiri mwingi.

Kwa kweli Yakobo alijengea Mungu wake madhabahu lakini mle Shekemu Yakobo alipata taabu nyingi sana. Jamii yake ilitawanyika. Binti yake Yakobo alipata mapenzi na mtu wa huko Shekemu. Huyo mtu alimnajisi Dina vibaya sana.

Wanawe Yakobo waliwaua watu wa Shekemu na kuwaibia mali yao, hivyo jina la Yakobo likaharibika mbele ya watu wa Shekemu.

  • Mhubiri Adrian Rodgers alisema, “dhambi itatupeleka mbali zaidi kuliko tunavyotaka kwenda. Dhambi inatuweka zaidi ya jinsi tulipenda kukaa, dhgambi inatugharimu zaidi ya jinsi tuko tayari kulipa.”
  • “Sin will take you further than you want to go, keep you longer than you want to stay and cost you more than you are willing to pay.”
  • Wengine wetu tumeona ukweli huu ukifanya kazi ndani ya maisha yetu. Umetembea mbali na Mungu lakini imekugharimu zaidi ya jinsi ulifikiri.
  • Mungu kwa neema zake anapenda sana umrudie kwa ukamilifu wote.
  • Mwanzo 35:1- “Mungu akamwambia Yakobo, ondoka, panda uende Betheli ukakae huko, ukamfanyie BWANA Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau ndugu yako.”
  • Mungu katika neema yake anamwita Yakobo mahali alipomwita safari ya kwanza. Mahali Mungu na Yakobo walipokutana uso kwa uso.
  • Wewe pamoja nami tulikutana na Yesu Kristo uso kwa uso, kwa imani pale msalabani.
  • Tunaporudi kwa Mungu tunarudi msalabani mahali pa wokovu, mahali pa ahadi.
  • Mwanzo 35:2-3- Yakobo alinena na jamii yake, “Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe, mkabadili nguo zenu. Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko, Yeye aliyenisikia siku ya shida zangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea.”
  • Hivyo Yakobo akapanga kurudi Betheli kukutana na Mungu. Lakini kwanza lazima kuondoa sanamu zote alizookota njiani.
  • Mwanzo 35:4- Je, mnao sanamu?

“Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, naye Yakobo akazificha chini ya Mwaloni ulioko Shekemu.”

  • Pete walizokuwa nazo masikioni mwao zilikuwa ni pete za hirizi na bahati, walikuwa bado kumtengea Mungu kwa imani.
  • Leo watu wanazo pete za miguu na vidole na masikio, na macho, na pua, na kitovu. Pete za hirizi haziwezi kazi- bali imani ndani ya Yesu Kristo.
  • Yakobo alizificha pete na sanamu zote mle Shekemu, wakatoka huko kwa imani pekee.
  • Mwanzo 35:5- “Wakashika njia, hofu ya Mungu ikashika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.”
  • Mungu aliwalinda kuliko pete na sanamu zao.
  • Mwanzo 35:6-7, Yakobo alimsikia Mungu akimwita, “Rudi kwangu.”
  • Yakobo alitupa miungu ya pete na sanamu zote na kumrudia Mungu BWANA WAKE.
  • Hivyo ndivyo tunahitaji kufanya kumrudia Mungu wetu kwa ukamilifu. Tunarudi msalabani hapo tulipokutana na Mungu mara ya kwanza.
  • Kama jinsi Yakobo, lazima kutupa sanamu zako zote, hirizi, pete, ulinzi na usalama wako, baraka na hatima yako iko kwa BWANA pekee.
  • Pengine unahitaji kuvunja uhusiano wako na wenye dhambi unao wategemea.
  • Leo rudi mpaka Betheli mahali ulipokutana na Mungu, mahali pa kuokoka, msalaba ndio asili ya mema.
  • Rudi mahali moyo wako ulikutana na Mungu mara ya kwanza.

MRUDIE BWANA

  • Juzi dunia yote ilisherehekea siku ya St. Patrick- Marchi 17.
  • Patrick aliandika kitabu kinachoitwa ‘Confenssions (maungamo).
  • Patrick aliazaliwa na kuishi Uingereza pwani yake. Babaye Patrick alikuwa mzee wa kanisa la kiagilikana.
  • Patrick alipokuwa miaka 16, walivamiwa na watu wa Ireland, hapo Patrick akachukuliwa mtumwa mpaka Ireland.
  • Patrick alifanya kazi ya kulisha nguruwe, siku moja neno la Mungu likamjia na St. Patrick akaokoka.
  • Bada ya kuwa mtumwa kwa miaka 6, Patrick alitoroka utumwa na kurudi Uingereza.
  • Katika mwaka wa (432 A.D) Mungu alimwita Patrick kurudi Ireland kuhubiri injili na kutetea haki za binadamu.
  • Patrick alirudi mahali alipokutana na Mungu mara ya kwanza- IRELAND.
  • Mrudie Mungu wako leo.

KUMBUKA AHADI ZAKE

  • Mrudie Mungu kasha mwache BWANA akukumbushe ahadi zake kwako- Mwanzo 35:9-10.
  • Mungu alimkumbusha Yakobo jina lake mpya.
  • Kitambulisho mpya na ahadi ya kumiliki- Mwanzo 35:11-15.
  • Utakapo mrudia BWANA Mungu wako, Mungu atakukumbusha ahadi zake kwako.
  • Mungu ni mwaminifu zaidi-2 Timotheo 2:13.
  • Kama jinsi mwana mpotevu-Luka 15:11-32- rudi kwa Bwana Mungu wako.

FANYA UPYA IMANI YAKO

  • Fanya upya imani yako upate nguvu za kupambana na shida zinazokuja mbele yako.
  • Tunaporudi kwa Mungu tunapata ujasiri wa kupambana na siku na magumu yajayo katika maisha yetu.
  • Tunapata nguvu ya kushindana na vita vyote vinavyokuja mbele zetu. Hivyo ndivyo Mungu alimfanyia Yakobo.
  • Mwanzo 35:8, “Akafa Deborah mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Mwaloni na jina lake likaitwa Alon-bakuthi” (Mwaloni mwa kilio).
  • Kumrudia Mungu si mwisho wa shida na mauti.
  • Yakobo amemrudia Bwana-Betheli, lakini Debora amekufa. Debora alikuwa mlezi wa Rebeka mamake Yakobo. Pia Debora alikuwa mlezi wa Yakobo na Esau.
  • Pamoja na mauti Yakobo alikuwa na tumaini kubwa katika BWANA.
  • Mwanzo 35:16-18.
  • Katika mauti na kilio Yakobo alipata nguvu katika ahadi za Mungu.
  • Mwanzo 35:19-20, “Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu. Yakobo akasimamisha nguzo (pillar) juu ya kaburi lake ndiyo nguzo la kaburi ya Raheli hata leo.”
  • Hii ilikuwa ni nguzo la tumaini. Bethlehemu ndio mahali alipozaliwa mwakozi wetu Yesu Kristo-Mathayo 2:1-6.
  • Mwanzo 35:21-29.
  • Hapa naye Isaka akafa. Yakobo alizika watu watatu kaburini tangu atoke Harani. Debora Raheli, Isaka.
  • Kumrudia Bwana si kusema kifo hakitakuja pamoja na kumrudia Kristo, kilio, mauti na shida zitakuwako, lakini Mungu anatupatia imani, tumaini na neema ya kuvumilia yanayotupata.
  • Hivyo, mrudie Bwana, wacha Bwana afanye imani yako kuwa timilifu ili uweze kustahimili yote yalio mbele ya macho yako.

MWISHO

  • Mrudie Mungu wako leo.
  • Wacha Bwana akupatie tumaini, neema na imani ya kupambana na yote yalio mbele yako.
  • Utakaporudi Betheli, fanya mwili wako na jamii yako kuwa El-Betheli, nyumba ya Mungu wako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “RUDI BETHELI.”

Leave a Reply to Micchael Paul Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *