RUTHU 1:1-22
UTANGULIZI
Imani aina saba zinapatikana katika maisha ya Imani ya wanawake saba katika Biblia. Ruthu– Imani inayo okoa, Esta-Kuishi kwa Imani, Mariamu-Magdalene-Kufuata kwa Imani, Mariamu dadake lazaro– Imani inayo abudu, Hanna– Imani inayo omba, Prisila– Imani ya kutumika, Sara– Imani ya kuwa na Jamii.
Ruthu alikuwa mwanamke wa Imani . Uamuzi wa Imani ndiyo iliamua maisha yake ya mbele kwa maana Ruthu alikuwa myahudi lakini mtaifa hakuwa chini ya agano ya Israeli (Waefeso 3:11-22) kwa maana Ruthu alikuwa chini ya laana mpaka kizazi cha kumi (Kumbu kumbu 23:3). Ruthu alikuwa kizazi cha kumi na moja (11) yaani kizazi cha neema.
Hebu Tuone:-
UAMUZI WA IMANI WA RUTHU KUOKOKA. (1:16)
- Ruthu aliamua kuokoka– Ruthu ali bandilika
- Elimeleki na Naomi mkewe walirudi nyuma wakahama bethlehemu kwa kwenda Moubu kwa sababu ya njaa nyingi (1:2)
- Wanawe Elimeleki, yaani Maloni na Kilioni waliwaoa wanawake wa Moabu, baadaye wote wawili wakafa (1:5)
- Naomi aliamua kurudi kwao, hivyo akamshauri ruthu kurudi kwa wazazi wake (1:15)
- Usipokee ushauri kutoka kwa watu waliorudi nyuma.
Ruthu alichangua mambo manne:-
i)Naomi
ii)Watu wa Naomi
iii) Mungu wa Naomi
iv)Inchi na Taifa ya Naomi (1:16-17)
2. Ruthu aliamua kwamba Mungu wa naomi atakuwa Mungu wake.
- Alichangua kuishi maisha mapya (v.16)
- Kuokoka ni kubadili hali ya maisha (Life style)
- Uamuzi kali unachangia Imani timilifu.
- “Watu wako ni watu wangu” (v.16)
- Ruth alijitoa 100% – Utakapokufa nami, na papo hapo nitazikwa.
- Mungu wa Israeli alikuwa lengo la uamuzi wa Ruthu- “Bwana anitende vivyo na kuzidi” v.17
- Ruthu alijitoa kufanya kazi kwa nguvu (2:2)
- Ruthu alifanya kazi kwa bidi sana (2:7)
- Ruthu alizalisha (2:19)
- Baraka za Mungu zinafuatana na uamuzi wa Imani.
- Aliongozwa na Mungu (2:3)
- Jicho la Boazi lilimpata Ruthu (2:5)
- Alikula mezani pa Boazi (3:13)
- Ruthu alipata kuolewa na Boazi (4:13)
- Uamuzi wa Imani sharti kuzaa matendo.
- Kuoga, kujipaka mafuta na kujivika mavazi mazuri (3:30
- Ruthu alichukua waajibu wa kuongea na Boazi (3:9)
- Vikwazo vitakuwapo (v.3:12)
- Mungu ataondoa vikwazo (4:6-14)
- Ruthu alipata neema– mtaifa– laana– alipata kibali Israeli.
- Ruthu alipata nafasi katika jamii ya Mwokozi wetu Yesu Kristo.
MWISHO
- Je, umeokoka ?
- Imani ya kuokoa ipo leo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
