Swahili Service

TUMEBARIKIWA NA BARAKA ZOTE ZA ROHONI.

MFULULIZO: WEFESO: YESU KRISTO NI YOTE NDANI YA YOTE.

SOMO: Wefeso 1:3.

 

Waefeso inatufundisha kwamba Yesu Kristo ndiye yote ndani ya yote. Ukimpata Yesu Kristo umepata yote. Kila mkristo ameitwa kutembea katika baraka zote katika Yesu Kristo. “Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”-Waefeso 1:3.

Tumeitwa kutambua na kutekeleza na kutembea katika ujazo wa baraka zote za rohoni, tuliopokea katika Kristo.

Mtume Paulo katika barua yake kwa Waefeso ametuongoza kufahamu yale Mungu ametufanyia katika Yesu Kristo-Vs. 3. Baraka zetu katika Yesu Kristo ni Pamoja na wokovu, msamaha, kufanywa kuwa wana, ukombozi, kibali, neema, Roho Mtakatifu, Hekima, njia ya kweli, tumaini ya milele na utukufu. Baraka hizi zote zinafikia katika kila eneo la maisha.

Wakristo wengi ni watupu kiroho, hawajafahamu uridhi wao ndani ya Yesu Kristo. Wengi hawakuishi sawa sawa na ukweli wa baraka hizi. Hebu tuone:-

MUNGU NDIYE KIINI NA CHANZO CHA KILA BARAKA ZA KIROHO.

  • Kila baraka ya kweli inaanza na Mungu.
  • Mtume Paulo hakutuongoza kwa hali yetu, mali zetu, kuitimu kwetu au mahusiano yetu na watu lakini ametuongoza kwa Mungu, baba wa mwokozi wetu Yesu Kristo.
  • Chochote Mungu anatupa ni dhibitisho ya neema yake, upendo, Hekima na wema wake.
  • Tunapoelewa kuwa Mungu ndiye kiini cha yote mema, hapo ndipo tunaacha kuwategemea wanadamu, na kuweka tumaini na ujasiri wetu kwa yeye asiyeweza kushindwa.
  • Mungu anaweza kuwatumia wanadamu kutubariki, lakini kiini cha baraka zako ni Mungu mwenyewe.
  1. Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo-1:3.
  • Paulo anatujulisha Mungu kama Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
  • Huyu Mungu baba ndiye baraka kwa mkristo.
  • Baraka zetu zinatoka kwa Baba anayeelewa na mahitaji yetu yote.
  1. Mwenye kupeana kila kipawa chema-Yakobo 1:17.
  • Kila kutoa kuliko kwema hutoka juu. Baraka zote zinatoka kwa Mungu.
  1. Mungu anatupa yote mema katika Kristo Bwana-Wafilipi 4:9.
  • Baraka zake ni kubwa katika mahitaji yetu.
  1. Mungu ni mwingi wa neema-2 Wakorintho 9:8.
  • Neema yake Mungu inatosha kwa kila changamoto, kila wajibu na haja zote.
  • Ibrahimu alibarikiwa awe baraka kwa wengi-Mwanzo 12:1-3.

BARAKA ZINAPATIKANA KATIKA KRISTO-Waefeso 1:3.

  • Baraka ni kwa Yesu Kristo, wala sio nje yake.
  • Mbali na Yesu Kristo hamna baraka za Mungu. Katika Yesu Kristo tumewekwa mahali pa kupokea baraka za Mungu.
  1. Tumekombolewa kupitia Yesu Kristo-Waefeso 1:7.
  • Katika Yesu Kristo tumepokea ukombozi kwa damu yake, msamaha wa dhambi.
  • Sasa dhambi haina nguvu juu yetu, sasa dhambi haina neno la mwisho juu yako.
  1. Tumekubalika kupitia Yesu Kristo-Waefeso 1:6.
  • Mungu anawafanya wakristo kukubalika katika Yesu Kristo.
  • Kukubalika kwetu mbele ya Mungu hakutegemei wanadamu au kanisa, dini na matoleo, lakini katika uhusiano wetu ndani ya Yesu Kristo.
  1. Tumekamilika ndani ya Yesu Kristo-Wakolosai 2:10.
  • Maandiko yanasema wakristo wamekamilika katika Yesu Kristo.
  • Yesu Kristo anatosha kwa msimamo wetu mbele za Mungu baba.
  1. Tumekuwa washindi katika Yesu Kristo-2 Wakorintho 2:14.
  • Mungu anatufanya washindi katika kila jambo.

TUMEPATA NJIA YA KUPOKEA UTAJIRI WA NEEMA YA MUNGU.

  • Baraka za kiroho tunaopokea kutoka kwa Mungu si za kutufanya kuwa na kiburi lakini ni za kumtumikia Mungu wetu.
  1. Neema ya wokovu-Waefeso 2:8-9.
  • Wokovu ni kwa neema kwa njia ya Imani, wala si kwa matendo yetu mema.
  • Wokovu ni uhusiano wako na Mungu wako.
  1. Neema ya kufunguliwa njia-Waefeso 2:18.
    • Sasa, tulio ndani ya Yesu Kristo, sisi sio wageni tena-tumepewa njia mwafaka ya kumjia Mungu.
  2. Neema ya kila hitaji-Waebrania 4:16.
    • Tumealikwa kumjia Mungu kwa ujasiri mkuu.
  3. Neema ya kutumika-1 Petro 4:10.
    • Kila mkristo amepewa kipawa cha kumtumikia Mungu na watu wake-1 Wakorintho 15:9-10.

NI LAZIMA TUTAMBUE NA KUTUMIA BARAKA ZETU ZA KIROHO.

    • Ujasiri usiojulikana hauwezi kutumika, hivyo ufahamu wa kiroho ni wa maana sana.
  1. Kufahamu kile Mungu ametupatia- 1 Wakorintho 2:12.
    • Roho Mtakatifu anatusaidia kutambua urithi wetu kiroho.
  2. Kukua katika ufahamu-2 Petro 3:18.
    • Tumeamrishwa kama wakristo kukua katika neema na ufahamu wa Mungu.
  3. Kutembea kwa Imani-2 Wakorintho 5:17.
    • Tunatembea kwa Imani.
  4. Kushikilia sana uzima wa milele-1 Timotheo 6:12.
    • Tukapate kushika sana uzima wa milele.

BARAKA ZA KIROHO ZINAHITAJI KUZAA MAISHA YA BARAKA.

    • Tumebarikiwa kubariki.
  1. Tumebarikiwa kuwabariki watu wengine-Mwanzo 12:2.
    • Tunawajibika kwa baraka tuliopewa kuwabariki watu wote na mataifa.
  2. Tumebarikiwa tukapate kuzaa matunda bora-Yohana 15:5.
    • Ishara ya kubarikiwa kiroho ni kuzaa matunda mengi.
  3. Tumebarikiwa tuwatumikie wengine-Mathayo 5:16.
    • Maisha yetu yanahitaji kuwaelekeza wengi kwa Yesu Kristo.
  4. Tumebarikiwa tupate kumtukuza Mungu-1 Wakorintho 10:31.
    • Kila baraka tuliopewa inahitaji kumtukuza Mungu aliye kiini cha baraka zote.

MWISHO

  • Leo amua kumfahamu Mungu wako, amini Ahadi zake, tembea katika kitambulisho chako ndani ya Yesu Kristo.
  • Uwe chombo cha baraka za Mungu kwa wengine.
  • Umebarikiwa katika Yesu Kristo, hivyo tembea kwa Imani, ishi katika utii, mtumikie Mungu kwa uaminifu, acha maisha yako yampe Mungu utukufu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *