II MAMBO YA NYAKATI 16
I WAFALME 15:9-24
UTANGULIZI
Jumapili iliyopita tulisoma juu ya mfalme Rehoboamu aliye pokea shauri kutoka kwa wajinga.Rehobohamu mwana wa mfalme Sulemani alimzaa mfalme Abija. Abija hakuwa tofauti sana na babaye. Lakini mfalme Asa alimpenda Mungu. Asa alianza vizuri lakini akamalizia vimbaya sana. Watu wengi wanasema hawawezi kufa kabla ya wakati wao kufika. Lakini Biblia inasema kwamba tunaweza kukata hau kuongeza miaka yetu kulingana na jinsi tunavyoishi maisha yetu. Adui asiyeongopa kifo ni adui mbaya sana. Imani yetu ni ya maana sana katika jambo hili. Biblia inasema kwamba mfalme Asa alikufa mbele ya wakati wake.
Hebu tuone kwanini alikufa mbele ya wakati wake (II Mambo ya Nyakati 16:12-14)
I. KWA NINI MFALME ASA ALIKUFA MBELE YA WAKATI WAKE.
- Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake.
- Ugonjwa wake ulizidi sana.
- Lakini Asa hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga.
- Kila mtu anaye watengemea madakatari na wanganga na kuwafanya Alpha na Omega ni mtu atakaye kufa mbele ya wakati wake. (Mhubiri 8:13)
- Haitakuwa heri kwa mwovu, wala hata zidisha siku zake; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.
- Mithali 10:27– Kumcha Mungu kwaongeza siku za mtu– miaka ya wasio haki itapunguzwa.
- Mfalme Asa alijitoa sana kwa madaktari na wanganga– alikataa kuomba.
- Asa hakujua kwamba X-ray na Ultra-sound haiwezi kuchunguza uchawi.
- Hata Daktari mwema anafahamu wakati wa kumshauri mgonjwa wake kuomba.
- Yesu Kristo aliwafufua wengi waliokuwa wamekufa mbele ya wakati wao.
- Adui shetani ana uwezo wa kufupisha maisha ya mtu.
- Wengi ambao Yesu aliwafufua kutoka kwa wafu walikuwa vijana– Lazaro, Dorkas alikuwa mke kijana, Kora, Dathani na Abiramu waliokufa jangwani walikuwa vijana.Ananiya na Sapphire walikuwa vijana, maana watoto wao hawajatajwa.
- Tazama (kumbukumbu 17:20)
- Njia mbili zimewekwa mbele yetu– njia ya mauti na njia ya uzima (Yeremia 21:8)- Mungu akitoa ulinzi wake kutoka kwetu mauti inatuandama karibu sana na shetani anapata nafasi (Yohana 10:10, Zaburi 103:3-5)
II. NGUVU ZA KAMALIZA (Power of the Terminators)
- Kuna nguvu zinazoitwa kamaliza hau maliza.
- Kazi ya kamaliza ni kumaliza watu.
- Nguvu za Usharati- (Sexual immorality) utoaji wa mimba umewaua wanawake wengi.
- Nguvu za Kufinyiliwa– oppression. Kitu kinacho kufinyilia moyo, hau katika ndoto.
- Magonjwa- (Infirmity) udhaifu
- Roho wa mauti na jihanamu– omba sana
- Nguvu za uchawi– wachawi wa leo si mama na wazee wakongwe, bali ni vijana, watoto na warembo, wasomi, wachungaji na wahubiri, wazee wakanisa, padre na wangwana!! Usikimbilie kushikwashikwa na salamu oyo oyo.
- Matamshi ya uovu– nguvu za mauti na uzima ziko kwa kinywa na ulimi– kataa sana maneno ya ndimi za watu. Kanusha !
- Nguvu za mapepo- (familiar spirits) wengine wanaweka agano na mauti kufa miaka ya 30 au 40 au 60. vunja agano za shetani.
- Nguvu za pembe tatu- (Triangular powers) ni agano na jua, mwezi na nyota (Zaburi 121)
- Hofu na fadhaha (Yohana 14:1) hizi mbili ni mauti ya karibu (Wafilipi 4:6-8)
- Ajali za karibu– (Tragedy activators)
- Wanaokunywa damu na kula nyama za watu (Zaburi 27:2)
- Roho ya mauaji, kujiua, laana za kumaliza jamii, agano za kifo, kuitwa na usiowajua, chakula mbaya, laana za mwenyewe etc.
III. JINSI YA KUZIDISHA MAISHA YAKO.
- Tubu dhambi zako, toa maisha yako kwa Kristo.
- Pokea ukombozi kupitia maombi ya Imani, kuvunja nguvu za kamaliza.
- Pokea ukombozi kupitia upako wa Roho mtakatifu.
- Tumia kanuni ya Roho Mtakatifu juu ya kanuni ya mauti (Warumi 8:2)
- Kariri (Zaburi 91), ndai neno la Mungu kila uamkapo na uendako.
MWISHO
- Usife mbele ya wakati wako !!
- Mungu atawaagiza malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
- Asa alikufa kwa kukosa kuomba
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025