SOMO: I WAFALME 1:1-53
UTANGULIZI
Je, wewe ni mtumwa wa yaliyopita? Ujumbe wetu leo ni kisa jinsi ya kuinuka juu ya yaliyopita pamoja na maovu uliyotendewa na watu.
Mfalme Daudi alipokuwa mzee na mkongwe, Sulemani kitinda mimba wake aliingia mahali pake. Ndugu yake Adonia alikuwa amejipandisha kuwa mfalme akawaalika wote kwa karamu ya kujiapisha lakini hakumwalika Sulemani. Babake Sulemani alikuwa mfalme Daudi, mfalme wa heshima sana. Lakini Daudi alianguka waajibu wake kama baba na mume. Pamoja na mke wake wa kwanza, yaani Mikali. Mfalme Daudi alikuwa na wake saba (2 Sam.15:16, I Nyakati 3:1-5) na mazuna kumi (10) wake sita aliowapata wakati wa uamisho (Exile) Hebroni na Beth-sheba alimnyanganya Uria mhiti huko Yerusalemu. Alikuwa na wana 10 kutoka kwa wake saba, wana wengine 9 na binti wengi sana.
Je, Sulemani aliwezaje kupambana na yaliyopita na kutazama yajayo?
Hebu tuone:-
I. JIWEKE HURU NA MAISHA YA KALE (I Wafalme 1:16-21)
- Ya kale yako na mikono mirefu sana usipo kata mikono yake.
- Ya kale inakumbuka sana kama hutayafuta katika akili yako. Sulemani hakuishi katika jamii bora na mazingira mazuri.
- Ndungu zake hawakumpenda. Vita, mauaji na unajizi ulikuwa kawaida katika nyumba ya ufalme.
- Dada– Nusu– yaani Tamari, binti wa mke wa tatu alinajisiwa na Amoni mwana wa mke wa kwanza.
- Absalomu naye alimuua Amoni. Baadaye Absalomu alimung’oa Mfalme Daudi kwa kiti cha enzi.
- Adonia naye alipambana sana na Sulemani kushindania ufalme (v.12,21)
- Sulemani alikuwa na mizigo ya kale lakini aliamua kutobeba ya kale na yakitambo.
- Sulemani aliazimia kutobeba shida za kizazi cha babaye.
- Haikuwa shida yake Sulemani kwamba wazazi wake walikuwa washerati na kwamba babaye alipenda wanawake na ndugu zake walikuwa wauaji.
- Imesemekana, mtu hawezi kuchangua wazazi wake, ndugu na dada zake, hau ukoo wake.
- Mfalme Sulemani alichangua kilicho chema-kusonga mbele.
- Hatuwezi kudharau ya kitambo lakini yajayo tunaweza kuyaunda.
- Hivyo tusiogope ya kale, utotoni, nyumbani na shida tulizopitia– Tazama yajayo.
II. JIWEKE HURU KUTOKANA NA JAMA ZA LEO (I Wafalme 38-40)
- Sulemani alikuwa na utabiri mzuri kutoka kuzaliwa.
- Katika kuzaliwa kwake, Sulemani, nabii Nathani alitumwa kumpa jina Jedidia hau “Mpendwa wa Mungu”
- Sulemani hakudai ufalme kama ndugu zake Absalomu na Adonia.
- Sulemani hakupigania ukuu, mamlaka na sifa, lakini Nabii, Kuhani na Jemedari walimtawaza Sulemani, Zadoki kuhani alimpaka mafuta na watu wote walishangilia mfalme wao (v.38-39)
- Adonia alipata aiubu kubwa maana aliachwa pekee.
- Sulemani alikuwa tofauti sana na baba yake Daudi.
- Daudi alikuwa mchungaji, askari na mwana siasa.
- Sulemani alikuwa mwenye hekima, philosophia na muamuzi. Daudi alitatua shida zake kijeshi, Sulemani alitatua shida kwa maaridhiano.
- Sulemani hakuwa kama ndugu zake, watu wa vita.
- Marafiki wa Daudi walikuwa Samweli, Joabu– Marafiki wa Sulemani walikuwa Nabii Nathani, Kuhani Zadoki na Benania.
III. JIWEKE HURU KUTOKANA NA KUHUKUMU WATU (I Wafalme 1:49-53)
- Sulemani hakuwa mtu wakulipiza kisasi na kumwanga damu kama baba yake Daudi.
- Sulemani hakuwaambia askari wake kumuua Adonia.
- Sulemani hakutumia njia ya kuua moja ndiposa wengine waogope, hau kuua kuku nyani waogope”
- Sulemani alikataa kumwanga damu. Sulemani alitumia uamuzi wake juu ya Adonia ona wake walienda kwa karamu yake.
- Sulemani alimpa Adonia nafasi ya pili.
MWISHO
- Yaliyopita na shida zake si shauri yako.
- Kila moja wetu ana fursa ya kuishi maisha yake, kuamua na dhamiri yake.
- Hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kununua moyo safi na dhamiri safi.
- Je, Umeokoka– Naomba, kamjie Mwokozi wako leo.
- Je, umekuwa mtumwa wa yaliyopita? Mpe Kristo maisha ya kale– Damu ya Kristo inaweza kukusafi.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025