Swahili Service

KUTOKA WAFU MPAKA HATIMA.

MFULULIZO: WEFESO: YESU KRISTO NI YOTE NDANI YA YOTE.

SOMO: WAEFESO 2:1-10.

 

Ujumbe wa leo unafundisha na kufunua jinsi neema ya Mungu inamtoa mtu kutoka kwa wafu na utumwa wa dhambi na kuingia katika wokovu, tumaini, shabaha, matendo mema na kuingia katika hatima ndani ya Yesu Kristo.

“Kwa maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”-Waefeso 2:10.

Waefeso 2:1-10, inatupa picha ya ajabu ya jinsi neema ya Mungu inafanya kazi. Kwanza, mtume Paulo anachora picha mbaya ya hali ya mwanadamu pasipo Yesu Kristo. “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu”-2:1.

Mauti ya kiroho maanake ni “kutengwa na Mungu na hali ya kukosa nguvu ya kuwa na uzima unaompendeza Mungu.”

Mtu anaweza kuwa hai kimwili, kufaulu katika maisha, masomo ya juu, Tajiri, mheshimiwa, mrembo, mwenye sifa, lakini amekufa kiroho, hawezi kumpendeza Mungu.

Paulo anatuonyesha jinsi tulivyokuwa pale kale, tulivyotendewa na neema ya Mungu, jinsi tulivyo sasa na jinsi tutakavyokuwa milele.

Kifungu hiki hakimaliziki na mauti, bali kunao “Lakini ya Mungu.” Lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda”-Vs. 4.

Rehema ya Mungu inaingilia kati wakati nguvu za mwanadamu zinafifia.

Mungu anawafufua wafu, anawapa uzima katika Yesu Kristo, anawaketisha Pamoja na Yesu Kristo katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo msamaha wa dhambi ni pamoja na kuwapa hatima katika Mungu.

Vs. 10, inatufunulia hatima ya wale wameokoka. “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”-Waefeso 2:10.

Mungu anayo sababu ya kutuokoa, amefufuka kutoka wafu, tukatembee na kufanya kazi njema iliyotengenezwa kwetu tangia awali. Hivyo, safari yetu ni kutoka mauti kuingia uzima, kutoka uzima kuingia kubadilishwa, kutoka kubadilishwa mpaka hatima. Hebu tutazame:-

DHAMBI INAZAA MAUTI NA KUTENGANA NA MUNGU.

  • Mtume Paulo anawajulisha waumini walipotolewa.
  • Bila Kristo tulikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zetu.
  • Mauti ya kiroho ilitutenganisha na Mungu na kuuvunja kabisa uhusiano wetu na Mungu.
  • Mapenzi ya mioyo yetu, tabia zetu na pia hatima yetu ilikuwa kinyume cha Mungu.
  • Kama si Mungu kuingilia kati, mwenye dhambi hawezi kutimiza lengo la Mungu kwa maisha yake.
  1. Tulikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zetu-2:1.
  • Dhambi inavunja uhusiano na ushirika na Mungu.
  • Mwanadamu anakuwa maskini, hawezi kutembea na Mungu.
  1. Tulitembea na kufuata kawaida ya ulimwengu-2:2
  • Tuliishi kulingana na mapokeo ya ulimwengu huu.
  • Kawaida ya ulimwengu huu ni kawaida ya dhambi.
  1. Tulitembea katika tamaa za miili yetu.
  • Tulitimiza mapenzi ya mwili na nia.
  • Tulikuwa Watoto wa hasira ya Mungu.
  1. Tulikuwa chini ya mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi-2:2.
  • Yesu Kristo ndiye anaweza kuvunja mamlaka ya giza na kutuleta katika hali ya maisha ya utii.
  • Mwana mpotevu alienda mbali na baba yake, akavunja ushirika na baba yake, “Alikuwa amekufa, lakini sasa yu hai”-Luka 15:24.

REHEMA ZA MUNGU ZINATUTOA KWA MAUTI NA KUTULETA KWA UZIMA.

  • Neno la maana katika Waefeso mbili (2) ni neno “Lakini Mungu”-2:4.
  • Mwanadamu alikuwa mfu, lakini Mungu alitenda kama Mungu.
  • Mwanadamu alitengwa, lakini Mungu akaleta upatanisho.
  • Mwanadamu hakuwa na nguvu na uwezo, Mungu alileta neema.
  • Wokovu unaanza na rehema za Mungu kupitia Yesu Kristo-Rehema ni upendo wa Mungu.
  1. Mungu ni mwingi (Tajiri) wa rehema-2:4.
  • Rehema za Mungu zinatufikia tusiostahimili.
  • Mungu hakutuacha katika dhambi na makosa yetu, alitujia.
  1. Mungu anatupenda sana-2:4.
  • Upendo mkuu wa Mungu ulimvuta kwetu tusiostahili wokovu wake.
  • Msalaba ndio asili na Ishara ya mema na upendo wa Mungu.
  1. Mungu alituuisha Pamoja na Kristo-2:4.
  • Injili inaleta ufufuo wa roho, waliokuwa wafu wanapokea maisha mapya kwa kuunganika na Yesu Kristo.
  1. Mungu anaokoa kwa neema-Waefeso 2:5-8.
  • Wokovu ni kipawa cha Mungu. Matendo ya mwanadamu hayawezi kulipia gharama ya wokovu.

NEEMA INABADILISHA MSIMAMO NA KITAMBULISHO CHETU-2:6.

  • Mungu, Pamoja na kutusamehe ametuamisha, ametufufua Pamoja na Yesu Kristo na kutuketisha Pamoja na Yesu Kristo.
  • Neema inabadilisha msimamo wetu kiroho.
  • Sasa hatumo katika hukumu, sasa hatujatengwa, tunaweza kumjia Mungu. Mfu, sasa ni mridhi wa kitambulisho kipya katika Kristo Yesu.
  1. Tumefufuliwa Pamoja na Yesu Kristo-Vs. 6.
  2. Tumeketishwa Pamoja na Yesu Kristo mbinguni.
  3. Tumefanyika viumbe vipya katika Kristo Yesu-2 Wakorintho 5:17.
  4. Tumeingia katika jamii mpya-Yohana 1:12.

MUNGU AMETUOKOA KWA SABABU YAKE-Waefeso 2:10.

  • Kila mkristo yuko na wajibu mbele za Mungu.
  1. Wewe sasa ni kazi ya Mungu. Wewe ni mradi wa Mungu. Dhamana yako hasa ni damu ya Yesu Kristo.
  2. Tenda matendo mema, tumikia, penda, shuhudia, eneza ufalme wa Mungu.
  3. Zaa matunda mema-Yohana 15:16.
  4. Mtukuze Mungu wako-Mathayo 5:16.

HATIMA INAHITAJI MAISHA MAPYA.

  • Hatima ya Mungu haiwezi kutimizwa kwa maisha ya kale.
  • Hatima ni kufanana na Yesu Kristo.
  1. Ishi katika upya wa uzima-Warumi 6:4.
  2. Badilisha nia na akili yako-Warumi 12:1-2.
  3. Jenga tabia mpya-Wagalatia 5:22-23.
  4. Uwe mwaminifu mpaka mwisho-Mathayo 24:13.
  • Vumilia na stahimili mpaka mwisho-2 Timotheo 4:7.

MWISHO

  • Safari ya kutoka mauti mpaka hatima inaanza na neema ya Mungu.
  • Tulikuwa wafu katika makosa na dhambi, tuliongozwa na tamaa ya mwili, lakini Mungu aliingilia kupitia upendo na rehema zake kwetu.
  • Mungu hakutuokoa twende mbinguni tu, lakini tumtumikie maana sisi tu kazi yake na mradi wake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *