MFULULIZO: WEFESO: YESU KRISTO NI YOTE NDANI YA YOTE.
SOMO: WAEFESO 1:4.
Ujumbe wetu wa leo unatufundisha kwamba kitambulisho, sababu, utakatifu na ujasiri wetu umepandwa katika uchaguzi wa Mungu kutuchagua katika Yesu Kristo.
“Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo”-Waefeso 1:4.
Huu ni ufunuo mkuu katika Imani ya mkristo. Huu ni ukweli wa Mungu, kwamba Mungu alitangulia kutuchagua kabla hatujakuweko. Hatukuingia katika jamii ya Mungu kuajali. Mungu alikuona kabla ya misingi ya dunia kuwekwa. Mungu anayafahamu yote (omniscient). Alikuona tangu jadi na akapanga wokovu wako, akafanya mipango yote ya makao yako mbinguni.
“Alituchagua katika yeye.” Uchaguzi wa Mungu upo katika Kristo.
Usalama wa wokovu wako katika Kristo haukuwa juu ya sura na msimamo wako, si kwa sababu ya kuhitimu au misimamo ya dini yako.
Mungu ametuleta kwa Yesu Kristo, hili tuwe watu wake, tuonyeshe tabia yake, tupate kutimiza malengo yake na kuishi kwa utukufu wake.
Kuchaguliwa na Mungu si jambo la kuwa na kiburi, lakini ni mwito wa kuishi takatifu, utii, utumishi na shukrani kwa Mungu.
Mungu hakutuchagua hili tuweze kuishi starehe, bali tuwe takatifu, bila mawaa katika pendo lake.
Kuchaguliwa na Mungu ni mwito wa kuishi katika utakatifu na kutii sauti yake. Hebu tuone:-
UCHAGUZI WA MUNGU ULIFANYIKA KATIKA MILELE.
- Paulo anatueleza kwamba Mungu alituchagua katika milele iliyopita kabla Mungu kuumba mbingu na dunia.
- Mpango wa Mungu kuokoa haukuwa jambo la dharura kwa sababu Adamu alianguka dhambi.
- Mungu alijua mahitaji ya mwanadamu, ndipo alipanga ukombozi kupitia Yesu Kristo kulingana na Hekima yake ya milele.
- Ukweli huu, unatupa ujasiri mkuu, kwamba uhusiano wetu na Mungu si ajali, bali wokovu wake umeunganika na mpango wa Mungu wa milele. Maanake maisha yako ni ya dhamani sana kiasi umekuwa katika mpango wa Mungu milele.
Ulichaguliwa kabla misingi ya uliwemngu-Waefeso 1:4.
- Mpango wa Mungu kuokoka ulikuweko mbele ya historia ya mwanadamu.
Uliitwa kwa makusudi na mpango wa Mungu-Warumi 8:28.
- Mungu anayafanya mambo yote kukutumikia kwa sababu unampenda Mungu na umeitwa kwa makusudi yake.
- Mambo yanaweza kubadilika lakini kusudi ya Mungu kwako haibadiliki.
Mungu alikufahamu tangu milele na milele-Yeremia 1:5.
Uliumbwa kwa utukufu wa Mungu-Isaya 43:7.
- Tangaza utukufu wa Mungu kote.
- Kusudi ya Mungu kwako ni tangu milele na milele-Yeremia 1:4-10.
MUNGU ALITUCHAGUA KATIKA YESU KRISTO.
- Mwito wa Mungu ni katika Kristo Yesu.
- Kila kitu kutoka kwa Mungu kinatujia katika Yesu Kristo.
Tumechaguliwa katika yeye-Waefeso 1:4.
- Kitambulisho chetu kiko katika Kristo Yesu.
- Kitambulisho chetu hakiko katika ukoo, kuitimu, majuto yetu au cheo.
Tumeitwa na Kristo-Yohana 15:16.
- Yesu Kristo alisema, “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kukaa…….”
- Mwito wa Mungu unakuja Pamoja na majukumu yetu mbele zake.
Tumekubalika katika mpendwa wa Mungu; yaani Yesu Kristo-Waefeso 1:6.
- Hatuhitaji dhibitisho kutoka kwa watu au dini juu ya kukubalika kwetu. Kibali ni kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo.
Tumekamilika katika Yesu Kristo-Wakolosai 2:10.
- Mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo amekamilika-hakuna cha kuongeza panapo Kristo.
- Yesu Krsito ametosha, kuokoa, kudumisha na kutosheleshwa.
KUCHAGULIWA NA YESU KRISTO NI MWITO WA UTAKATIFU-Waefeso 1:4.
- Tumeitwa kuishi katika utakatifu, bila mawaa katika pendo.
- Ni lazima tuwe kama Yesu Kristo-watakatifu.
Tumeitwa kuwa watakatifu-1 Petro 1:15-16.
Tumeitwa kuishi maisha safi-2 Wakorintho 7:1.
- Ni lazima kuacha tabia mbaya.
Tumeitwa kutembea katika nuru-1 Yohana 1:7.
- Maisha ya kuchaguliwa na Kristo na maisha ya ushirika na Yesu Kristo, ni maisha wazi, maisha bila giza.
Tumeitwa kuishi maisha yasiyo na hatia-Wafilipi 2:15.
- Tumeitwa kung’ara kama Nyota za anga katika ulimwengu wa giza.
- Tabia zetu zinahitaji kuwavuta watu kwa Kristo-2 Wakorintho 5:17.
KUCHAGULIWA KUNATUPA KITAMBULISHO KIPYA.
- Watu wengi wanaruhusu maisha yao ya kale kukataliwa, kutofaulu, maisha ya jamii zao, na Mawazo ya watu kuwapa kitambulisho.
- Lakini mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo anapata kuwa kiumbe kipya.
- Tunapochaguliwa hatutegemei tena watu na mafikira yao. Sisi ni kile Mungu anatuita-wana wa Mungu.
- Dhamana yako ni ile dhamana Mungu amekupa, katika Kristo. Dhamana yako ni damu ya Kristo.
- Sasa tunaishi juu ya jukwaa ya kibali cha mwanadamu.
Mzao mteule-1 Petro 2:9.
- Ndani ya Yesu Kristo tumekuwa mzao mteule ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu.
- Tupate kutangaza Fadhili zake yeye aliyetuita kutoka gizani, tukaingie katika nuru yake ya ajabu.
Viumbe vipya-2 Wakorintho 5:17.
Wana wa Mungu-Yohana 1:12.
Warithi wa Mungu-Warumi 8:16-17.
MWISHO
- Kuchaguliwa ndani ya Yesu ndio mwito mkuu zaidi katika Mungu.
- Kabla misingi ya dunia kuwekwa, Mungu alikufahamu na kukuita ukawe mwana wa pendo lake.
- Katika Yesu Kristo tumepata kitambulisho mpya.
- Leo, ishi kama mwana wa Mungu, kataa maisha ya dhambi, kataa kukataliwa na watu, kataa kuishi sawa sawa na mafikira ya watu wa dunia hii.
- Waambie ya kwamba umechaguliwa na Mungu na kukubalika mbinguni na kibali cha Mungu ni tosha.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- TUMECHAGULIWA KATIKA YESU KRISTO - November 1, 2026
- FREE TO BE FREE - November 1, 2026
- TUMEBARIKIWA NA BARAKA ZOTE ZA ROHONI. - October 25, 2026
