Series Swahili Service TIMOTHY

MAHALI PA MWANAMKE

I TIMOTHEO 2:9-15

UTANGULIZI

Kuna maono mengi sana juu ya mahali pa          mwanamke kanisani na katika maisha. Kuna wanaume wanao fikiri mahali pa mwanamke ni    chini ya miguu yao, lakini hayo si mafundisho ya Biblia. Wanaume wengine wanapanga mwanamke sehemu yake ni kukaa na kwenda bila viatu na kila wakati kuwa na mimba (barefoot and pregnant) lakini hayo si mafundisho ya Biblia. Mimi           nawapongeza wanawake wote na zaidi wanawake wa FBC/AR. Kuna shule mbili duniani, hizi shule za mawazo zinatawala juu ya kazi na sehemu ya wanaume na wanawake.

  1. Wanawake na wanaume ni sawa katika kila hali maishani (Egalitarianism) huu ndio msimamo wa wanawake wa kisasa (Feminism). Kulingana na shule hii wanawake na wanaume wako na haki ya kuhubiri, kuwa wazee na mashemazi (Deacons) wachungaji, asikofu. Shule hii inasimama juu ya maandiko kama vile Wagalatia 3:28.
  2. Wanawake na wanaume waliumbwa sawa lakini jukumu ni tofauti (Complementarianism) utofauti wa wanawake na wanaume unatufanya kutengemeana hivyo wanawake na wanaume ni sawa kabisa kiroho katika Kristo lakini kazi tofauti– Huu ndio msimamo wa Biblia na Mtume Paulo (Mwanzo 2:18). Mwanamke anamkamilisha mume na mwanaume anamkamilisha mwanamke (Mwanzo 2:18-25)

Dhambi ilipoingia duniani kazi na wajibu wa mume na mke ilibadilika– lakini si mbele ya Mungu– lakini mbele ya wanadamu (Mwanzo 3:16)

Dhambi ilifanya mwanamke kuwa mshinani na   mpizani. Mwanamke sasa, mapenzi yake ni kumtawala mume. Dhambi ilimfanya mwanamme mtawala kuwa mkali juu ya mke, hivyo mwanamme mapenzi yake ni kutawala kwa nguvu zote (domineering and absolute control) Haya hayakuwa mapenzi ya Mungu kamwe.Mwanamke alitolewa kutoka mbavuni, si miguu hili kukanyangwa, si kichwa hili kutawala, lakini karibu na moyo ili mume ampende na kumlinda mkewe. katika ulimwengu wa kale, wanawake hakuwa na haki, lakini walikuwa mali ya wanaume– ngumu sana. Katika Uyahudi wanawake walikuwa sawa (Kumbu.1:1, Kutoka 21:28-32) wanawake walikuwa na haki ya mali (Hesabu 36:12) Ibada (Kutoka 12:3,Kumbu 16:9-15) Nadhiri (Hesabu 36:12) kazi (Kutoka 38:18, Neh.7:67). Mungu alifanya kazi moja kwa moja na wanawake (Mwanzo 3:13, 16:7-13, Waamuzi 13:3) Injili ilipokuja , mahali pa wanawake ilikuwa juu zaidi.

Hebutuone:-

I.  MWANAMKE WA KIUNGU NA USHUHUDA WAKE (I Tim.2:9)

Paulo alimwandikia Timotheo akiwa pale Efeso.

  • Efeso palikuwa mahali pa upagani. Mungu wa kike yaani(Diana) aliabudiwa pale. Wanawake 1000 walikaa hekaluni la Diana kama kahaba wa hekalu.
  • Wanawake wa Efeso walipokuja kuokoka walikuja na mavazi ya ki-Diana kanisani pamoja na desturi za upangani kanisani. Hivyo Paulo anawafundisha wanawake wakristo kuwa tofauti.
  • Hivyo wanawake wasivae mavazi hili kujionyesha hau kwa kuwavutia wanaume, lakini wavae vizuri kumpendeza Mungu.
  • Ushuuda wa mwanamke kanisani– matendo mema (I Petro 3:1-6)
  • Utu wa ndani ni muhimu zaidi kuliko inje.

II.  MWANAMKE WA KIUNGU NA MAFUNDISHO YAKE (11-12)

  • Wanawake wasitengwe na mafundisho kanisani
  • Zamani wanawake hawakuruhusiwa kuingia ibada.
  • Lakini wanawake wanapoingia ibada wajifunze katika utulivu– si kama kwa Diana.
  • Wanawake wanao nafasi kubwa kufundisha kanisani, kufundisha wanawake, watoto, wanaume moja kwa moja (Matendo 18:26)
  • Wanawake wazee wawafundishe wanawake vijana (Tito 2:3-5)
  • Wanawake wazee waishi maisha ya utakatifu– Kama Kristo.
  • Wanawake waishi maisha ya kweli (Honesty) bila masengenyo.
  • Wanawake waishi maisha ya kiasi (sober) wasiwe walevi.
  • Wafundishwe maisha ya ndoa na nyumba.

III. MWANAMKE WAKIUNGU NA KAZI ZAKE

Mwanamke awe mwenye ibada (I Wakorintho 11:2-16)

  • Mama Timotheo na nyanya Wake walikuwa wanawake wa ibada (2 Tim.2;15)
  • Hanna alikuwa mwanamke wa ibada (I Sam 1:9-28)
  • Anna alikuwa mwanamke wa ibada hekaluni (Luka 2:36-37)
  • Ibada inamaanisha kumjua Mwokozi kama Bwana na Mwokozi kibinafsi.

Mwanamke awe mfanya kazi wa Mungu (Warumi 16:1)

  • Fibi alikuwa mtenda kazi pamoja na Paulo katika kanisa la Kenkrea.

Mwanamke awe mshahidi (I Petro 3:1)

  • Mwanamke aliyeokoka haubirie mume wake aliye bado kuokoka.

Mwanamke askari wa Kristo (Matendo 1:4; 12:2) na zaidi katika maombi.

  • Kuna kazi nyingi ya wanawake wakristo kanisani na inje ya kanisa.

 

MWISHO

  • Ninamtukuza Mungu kwa ajili ya wanawake wa kanisa hii na kazi yao kwetu kama kanisa.
  • Kama bado hujaokoka nafasi hipo kwako leo.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “MAHALI PA MWANAMKE”

Leave a Reply to Jaffery wesanzaj@gmail.com Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *