MFULULIZO: MAPAMBANO YANAOBADILISHA HATIMA.
SOMO: MWANZO 32:24-30.
Mapambano ya kweli na Mungu yanabadilisha kitambulisho, tabia na uhusiano wa mtu na Mungu.
“Akamwambia, jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”-Mwanzo 32:28.
Katika Biblia yote mapambano na Mungu yanaleta mageuzi katika watu wa Mungu. Haya mapambano si ujuzi wa kawaida, lakini ni nyakati Mungu anakutana na mtu uso kwa uso na hana kwa hana. Yakobo alikutana na Mungu uso kwa uso pale Penueli.
Yakobo alikuwa ametumia miaka nyingi akijitegemea, akitegemea akili zake, ujanja wake, maarifa yake na juhudi zake binafsi.
Hata ingawa Yakobo alikuwa amepokea ahadi za Mungu, Yakobo alijaribu sana kutimiza ahadi za Mungu kwake kwa njia ya kibinafsi. Sasa, Yakobo alipanga kukutana na ndugu yeke Esau baada ya miaka nyingi.
Hapa Yakobo alijaa hofu na hali ya kutofahamu yatakaojiri juu ya maisha yake na jamii yake. Ilimpasa Yakobo kuutafuta uso wa Mungu ki ndani zaidi.
Penueli ndio mahali maisha ya Yakobo yalibadilika milele.
Yakobo aliingia katika hayo mapambano kama “Yakobo” (mdanganyifu) na akatoka pale kwa jina mpya yaani “Israeli” maanake “mwana wa ufalme na Mungu,” “A prince with God.”
Kila mtu wa Mungu anahitaji kuwa na kila “Penueli ya binafsi.” Pale Penueli ni mahali ubinafsi unavunjika, imani inajengwa na kutiwa nguvu, hapo Penueli hatima ya mtu inabadilishwa na nguvu za Mungu na uwepo wa Mungu unakuwa dhahiri. Hebu tutazame:-
MAPAMBANO NA MUNGU YANATOKEA WAKATI NA MAJIRA YA MGOGORO (CRISIS).
- Mungu anatumia nyakati na majira magumu katika maisha kuongea na watu wake.
- Nyakati za mgogoro Mungu anatoa nafasi ya mageuzi na mabadiliko.
Mgogoro unafichua mahitaji yetu ya Mungu-Mwanzo 32:6-12.
- Yakobo aliogopa sana aliposikia Esau anakuja kukutana naye akiwa na jeshi la watu 400.
- Hofu yake Yakobo ilimfanya kuutafuta uso wa Mungu katika maombi na tegemeo lake juu ya Mungu.
- Yakobo alijua kwa nguvu zake hawezani na ndugu yake Esau.
Mungu anatumia nyakati ngumu kunena na nafsi zetu-Zaburi 119:71.
- Dhiki inamtoa mtu kutoka hali ya kujitegemea. Hapo mtu anaacha kujitegemea na kutafuta uwepo na mwelekeo wa Mungu.
Kujitenga na watu kunaleta ushirika na Mungu-Mwanzo 32:24.
- Yakobo aliachwa peke yake mbele ya kupambana na Mungu.
- Kujitenga kunamwalika Mungu kupambana na nafsi zetu.
Mungu anawajibu wale wanaomtafuta kwa dhati-Yeremia 29:13.
- Hapa Yakobo alikuwa katika changamoto iliyokuwa kubwa zaidi katika maisha yake.
- Yakobo alipambana na Mungu, hofu zake zote zilikwisha, Mungu alimpa hakikisho na baraka-Mwanzo 32:24-30.
MAPAMBANO YA KWELI NA MUNGU YANABADILISHA KITAMBULISHO CHAKO.
- Mungu hamwachi mtu bila mabadiliko ikiwa, mapambano yako na Mungu ni ya kweli.
- Mungu anabadilisha sababu ya kuishi, tabia na kitambulisho kiroho.
Mungu anakabidhi utu wetu wa kale-Mwanzo 32:27.
- Kabla Mungu hajageuza jina la Yakobo, ilibidi Yakobo kukubali hali yake ya hapo kale.
- Kuungama kwa kweli ndicho chanzo cha mageuzi ya nafsi.
Mungu anapeana kitambulisho kipya-Mwanzo 32:28.
- Yakobo akawa Israeli, kumaanisha majira mapya ya mamlaka, kibali na Agano na Mungu.
Mabadiliko yanaanza ndani-2 Wakorintho 5:17.
- Wanaopambana na Yesu Kristo wanapata kuwa viumbe vipya.
- Mungu kwanza anabadili maisha ya ndani kabla ya maisha ya nje.
Mungu anarejesha sababu ya asili na ile ya kwanza-Waefeso 2:10.
- Kila pambano na Mungu linarudisha mtu kwa mpango wa Mungu.
- Abramu alibadilishwa akawa Ibrahimu. Mungu alibadili jina lake, hatima yake, akamfanya baba wa mataifa mengi.
MAPAMBANO NA MUNGU YANAHITAJI IMANI YA KUSTAHIMILI.
- Yakobo alikataa kumwacha Mungu mpaka Mungu apate kumbariki.
- Wanaopenda mabadiliko ya kudumu lazima kuvumilia katika kumtafuta Mungu.
Kataa kushindwa na maombi yako-Luka 18:1-8.
- Maombi ya kudumu na kustahimili yanaonyesha imani yako kwa Mungu.
Shikilia sana ahadi za Mungu-Waebrania 10:23.
- Waumini lazima wawe na ujasiri, Mungu atatimniza ahadi zake-Waebrania 10:23.
Kustahimili kwa kiroho kunaleta kupenya-Mwanzo 32:26.
- Yakobo alimwambia Mungu, “Sitoki hapa na sikuachilii mpaka utakaponibariki.
- Imani kamilifu inastahimili mpaka kupata matokeo.
Imani ya kweli inapata dhawabu-Waebrania 11:6.
- Mungu huwapa dhawabu wamtafutao.
KILA MAPAMBANO YA KWELI YANAZAA USHINDI WA KUDUMU.
- Mapambano ya kweli kati ya mtu na Mungu yanakuwa na ushuhuda katika maisha.
- Mabadiliko katika tabia, utii na usawishi wa kiroho.
Maisha na mwelekeo yanabadilika-Mwanzo 32:31.
- Yakobo alichechemea kwa sababu paja lake liliumia daima.
Uhusiano wako na Mungu unabadilika-Mwanzo 33:1-4.
- Mapatano ya Yakobo na Esau yaliwezekana kwa sababu ya Penueli.
Ushuhuda wako utawabariki wengi-Zaburi 66:16.
- Wanao okoka kweli wanakuwa shuhuda hai ya kuwasaidia wengine.
Hatima yako itatimiza makusudi ya Mungu kwa maisha yako-Warumi 8:28-30.
MWISHO.
- Mapambano ya Yakobo na Mungu mle Penueli inatukumbusha wakati mfupi katika uwepo wa Mungu unabadilisha maisha milele.
- Kila Mkristo anahitaji kutafuta sana mapambano yake na Mungu-Penueli ya binafsi.
- Mungu anapo pambana nawe, hofu inakuwa imani, udhaifu unakuwa nguvu na hatima yako inaenda sambamba na mapenzi ya Mungu.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUSA MBELE YA KIJITI KILICHOWAKA MOTO. - October 18, 2026
- DISCOVERING GOD’S PURPOSE FOR YOUR LIFE - October 18, 2026
- FAITH IN THE FACE OF CHALLENGES - October 14, 2026
