Swahili Service

YESU KRISTO NDIYE HAKI YETU

MFULULIZO: UFUNUO WA YESU KRISTO.

SOMO: 1 WAKORINTHO 1:30; WARUMI 3:21-26.

 

Ujumbe kwetu leo ni kwamba Yesu Kristo ndiye kiini cha haki yetu mbele za Mungu baba. Tunahesabiwa haki si kwa sababu ya Matendo yetu mema lakini kwa njia ya imani ndani yake Yesu Kristo.

“Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi; kusudi kama ilivyoandikwa, yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana”-1 Wakorintho 1:30-31.

Haki ni msingi wa uhusiano wa kweli na Mungu, lakini tangu mwanadamu alipoanguka katika dhambi, mwanadamu alipoteza nguvu za kusimama mbele ya Mungu Mtakatifu.

Hakuna kiasi cha kazi chema tunaweza kufanya. Hakuna Matendo ya dini yanaweza kutusaidia. Hakuna uzuri na nidhamu tunaweza kuwa nazo, hakuna juhudi tunaweza kufanya tupate kukubalika na Mungu tupate kurudi katika hali ya kwanza ya Adamu. Iligharimu dhabihu ya damu ya Yesu Kristo mwana wa Mungu-Mwana wake wa pekee, asiye na dhambi.

Tunaposema “Yesu Kristo haki yetu” tunao maana kwamba kwa kifo chake msalabani na kufufuka kwake Yesu Kristo alibadili dhambi zetu na kuzilipia ili tupate haki yake.

Tunampomfahamu Yesu Kristo kuwa haki yetu, uhusiano wetu na Mungu unabadilika. Sasa hatusumbuki tena kujipendekeza kwa Mungu, bali tunapumzika katika kazi Yesu Kristo alitekeleza pale msalabani na kuimaliza ile kazi.

Ufunuo wa haki ya Mungu unatupa nguvu za kuishi maisha takatifu, maisha ya ushindi. Sasa hatutegemei nguvu za mwili, tunategemea neema ya Mungu ikifanya kazi ndani yetu. Hebu tujifunze:-

YESU KRISTO KIINI CHA HAKI YETU.

  • Haki ya kweli inatoka kwa Yesu Kristo peke yake.
  • Bila Yesu Kristo mwanadamu anazidi kuishi maisha ya hukumu na kuwa mfu kiroho.

Chipukizi la haki-Yeremia 23:5-6.

  • Yesu Kristo kiunabii anaitwa “Bwana haki yetu.”
  • Yesu Kristo pekee ndiye anao nguvu na mamlaka ya kuwahesabia wanadamu haki mbele za Mungu.

Haki inafunuliwa na imani-Warumi 3:21-22.

  • Haki ya Mungu inafunuliwa kwa njia ya imani ndani ya Yesu Kristo wala si kwa njia ya sheria au kazi ya mwanadamu-Warumi 3:21-22.

Haki kama kipawa-Warumi 5:17.

  • Kupitia Yesu Kristo, tunapokea kipawa cha haki bure. Kipawa cha haki hakifanyiwi kazi, bali kinapokelewa kwa neema.

Mabadilishano mle Kalvari-2 Wakorintho 5:21.

  • Yesu Kristo hakuijua dhambi, lakini alifanyika kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
  • Mwivi pale msalabani alihesabiwa haki si kwa Matendo yake mema, lakini kwa sababu ya imani yake ndani ya Yesu Kristo-Luka 23:42-43.

HAKI INAPEANWA, HAIWEZI KUFANYIWA KAZI.

  • Haki ya kupewa Maanake ni kwamba Mungu anawahesabia haki ya Yesu Kristo wale wamwaminio.

Juhudi za mwanadamu hazitoshi-Isaya 64:6.

  • Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo isiyotiwa unajisi.
  • Utakatifu wa mwanadamu huwezi kuwa umepugukiwa na utukufu wa Mungu.

Haki kwa njia ya imani-Warumi 4:3-5.

  • Ibahimu alimwamini Mungu, ile imani yake ilihesabiwa kuwa mbele za Mungu.
  • Haki inapatikana kupitia imani.

Mwisho wa sheria ni haki-Warumi 10:4.

  • Yesu Kristo alitimiza sheria yote, hivyo sisi tulio ndani ya Yesu Kristo hatutegemei tena Matendo ya sheria, bali tunategemea kazi aliyomaliza Yesu Kristo msalabani na kaburini alipofufuka kwa wafu.

Leo tunasimama tumehesabiwa haki mbele za Mungu.

  • Tulihesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya imani, sasa tumepata amani na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu-Warumi 5:1.
  • Mtume Paulo alihesabiwa haki si kwa matendo yake bali kwa imani yake ndani ya Yesu Kristo-Wafilipi 3:8-9.

HAKI UZAA UTAKATIFU.

  • Yesu Kristo anapokuwa haki yetu, asili yake inazaliwa ndani ya maisha yetu, tabia na mienendo yetu inabadilika na kufanana na ile ya Yesu Kristo.

Tunda la haki-Wafilipi 1:11.

  • Haki inazaa utauwa, tabia nzuri na Matendo mema yanayo mpendeza Mungu.

Nguvu za kushinda dhambi-Warumi 6:18.

  • Tunawekwa huru kutokana na dhambi.
  • Tunapata kuwa watumwa wa haki huku tukiishi katika ushindi juu ya dhambi.

Dirii ya haki (breastplate)-Waefeso 6:14.

  • Haki inamlinda mwenye kuamini kutokana na hukumu na kuhukumiwa na dhamiri.

Mwito wa kuishi katika mazoea ya haki-1 Yohana 3:7.

  • Anayefanya haki ndiye mwenye haki kama jinsi Yesu Kristo aliye haki.
  • Haki ya kweli ni ya msimamo na pia hali ya kuendelea (positional and progressive).
  • Nabii Danieli aliishi chini ya mamlaka ya wenye dhambi-Danieli 6:10-23.

HAKI INALETA DHAWABU YA MUNGU NA MAMLAKA YAKE.

  • Kuishi chini ya haki ya Yesu Kristo inatupa ujasiri, kibali na baraka za Mungu.

Ujasiri mbele za Mungu-Waebrania 4:16.

  • Kwa sababu ya haki ya Yesu Kristo tunaweza kumkaribia Mungu kwa ujasiri mwingi bila hofu.

Tunalindwa kutokana na hukumu za watu-Isaya 54:17.

  • Hakuna silaha au hukumu inaweza kusimama mbele ya wao waliohesabiwa haki na mkombozi wetu Yesu Kristo.

Baraka za haki-Zaburi 5:12.

  • Mungu anawazingira wenye haki kwa kibali kama jinsi ngao.

Dhawabu ya milele-1 Timotheo 4:8.

  • Taji ya haki inawangojea wale watakao kaa wakiwa waaminifu mpaka mwisho.
  • Haki ya Ayubu ilimpa ulinzi na baadaye Mungu alimpa urejesho-Ayubu 42:10-12.

MWISHO

  • Yesu Kristo sio tu Mwokozi wetu, lakini yeye pia ni haki yetu. Ndani yake tumehesabiwa haki, tumetakaswa na tumekubaliwa haki, tumetakaswa na tumekubalika mbele ya Mungu.
  • Ujasiri wetu haumo katika Matendo yetu, bali ujasiri wetu humo katika kazi aliyomaliza.
  • Tunapotembea katika ukweli huu, hukumu unapoteza nguvu zake nasi tunapata kuishi katika huru na neema.
  • Basi tukadumu katika Kristo, tukajivike haki yake, tukaishi katika utakatifu.
  • Mungu anapotutizama kupitia kwa Yesu Kristo, anatuazimia na kututangaza haki, tumesamehewa dhambi zetu na kuwekwa huru kabisa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *