MFULULIZO: TUMAINI HAI. SOMO: 1 Petro 2:11-25. Kunyenyekea ndilo neno linalochukiwa sana duniani. Wengi wetu tunafanya kama jinsi kijana mmoja alivyolazimishwa na mama yake kuketi chini. “Johnny tafadhali keti chini.” Johnny alipokataa kuketi chini, mamake alitumia nguvu kumketisha chini. Ndiposa alipoketi alimwambia mamake, “Mama hata ingawa nimeketi kimwili, lakini katika roho yangu ningali nimesimama.” …
Category: Swahili Service
VIKUMBUSHO KWA WASAFIRI NA WAGENI
MFULULIZO: TUMAINI HAI. SOMO: 1 Petro 2:9-12. Mtume Petro anawaeleza waumini kwamba sisi NI WASAFIRI NA WAGENI duniani. Mgeni maana ni mtu anayeishi kwa muda katika nchi isiyo yake. Huyu mgeni ameishi katika nchi ya kigeni kwa muda kiasi amehitaji kuwa na nyumba ya kuishi na kufanya kazi lakini katika nchi ya ugeni. Lakini …
WOKOVU WETU MKUU
MFULULIZO: TUMAINI HAI. SOMO: 1 PETRO 1:10-12. Mtume Petro amekubali kwamba wakristo wa kwanza wametawanyika pote wakihofia maisha yao. Hawa Wakristo amewahimiza kwamba wakafurahi sana hata katika mateso. Amewaeleza kwamba wamepata urithi mkuu katika Kristo. Mateso ni kwa muda mfupi tu, tukilinganisha na urithi tuliopata katika Yesu Kristo. Petro amewapongeza sana kwamba hata ingawa …
TUMAINI HAI
MFULULIZO: 1 PETRO-YESU KRISTO, TUMAINI LETU. SOMO: 1 PETRO 1:1-12, WAEBRANIA 11:1 Yesu Kristo yu hai, basi uwe na hakika na furaha hata wakati wa shida na mateso. Furaha hata wakati wa shida na mateso. Mtume Petro aliandika kwa wakristo waliokuwa katika uamisho, wametapakaa kote katika Asia Minor (Asia Ndogo). Mahali sasa ni Uturuki kaskazini. …
KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI
MFULULIZO: MKARIBU MUNGU. SOMO: ZABURI 42:7 (42:1-11). Wakristo wengi wanafurahi kukaa katika maji ya ufuoni. Wengi hawapendi kuingia ndani zaidi na kumfahamu Mungu wao. Ukristo wa namna hii hauleti mabadiliko na ukaribu na Mungu. Lakini Mungu anatuita kuingia mpaka kilindini, kilindi cha ibada, kilindi cha maombi, kilindi cha neno, kilindi cha shabaha na lengo, …
KUKAA KATIKA MAHALI PA SIRI
MFULULIZO: KARIBU NA MUNGU. SOMO: ZABURI 91:1. Kukaa katika mahali pa siri pake aliye juu ni mwaliko wa kupokea utimilifu wa uwepo na amani ya Mungu. Hapa ni mahali pa mawasiliano ya karibu na Mungu, hapa utapata kuongozwa na kupewa nguvu za Roho Mtakatifu-Zaburi 91:1, “Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika …
MKARIBISHE MUNGU KWA KARIBU
MFULULIZO: KARIBU NA MUNGU. SOMO: YAKOBO 4:8. Kumkaribia Mungu si jambo la kufanya mara moja tu, lakini ni safari ya kuendelea kuutafuta uso wake, kwa moyo wako wote. Kumkaribia Mungu ni moja wapo ya nidhamu za imani ya Kikristo. Kumkaribia Mungu ni njia ya kujenga uhusiano wa karibu na Mungu kwa unyenyekevu wote, kujitoa …
CHIMBUA VISIMA YA MAOMBI
MFULULIZO: KUPENYA KUSIO KWA KAWAIDA SOMO MWANZO 26:18; MARKO 16:15-20 Ikiwa tutapata kuwa na nguvu, ishara maajabu, uponyaji na miujiza kama kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ni lazima kuweka maombi katika mstari wa kwanza kama wao. “Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale …
MACHOZI YA MWOKOZI JUU YA WALIOPOTEA
SOMO: LUKA 19:41-44 Leo ni Jumapili ya Mitende, yaani, “Palm Sunday.” Siku kama hii miaka 2,000 iliopita Mwokozi wetu Yesu Kristo aliingia mji wa Yerusalemu huku akijua anaenda kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na milele. Yesu Ndiye Mwokozi yule aliyelia siku hiyo kwa ajili ya …
UTABIRI WA MWISHO KUTOKA KWA MUNGU
MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU. SOMO: DANIELI 12:1-13. Leo hii tunatamatisha mfululizo wa jumbe katika kitabu cha Danieli. Danieli sura ya 12 ndio mwisho wa unabii aliyepewa nabii Danieli. Kuna ukweli tano katika sura ya 12. Huu ni ukweli wa Mungu juu ya mwisho wa historia ya mwanadamu duniani. Hebu tutazame:- UKWELI WA MUNGU: KUNA …
